TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO
Mwambawahabari
wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah
Mwandumbya (katikati) akitoa maagizo kwa uongozi wa Kiwanda cha Manyara
Sugar Company Limited kuhusu kutoa takwimu sahihi uzalishaji sukari
wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za
Wafanyabiashara.
Na. Rachel Mkundai, Manyara
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara
wenye viwanda vya kutengeneza mali ghafi za kutengenezea pombe kali
kutoa tawimu sahihi ya kiasi kinachozalishwa na mahali inapouzwa ili serikali iweze
kukusanya kodi yake stahiki kupitia pombe kali.
Hayo yamesemwa na Kamishna waKodi za Ndani wa TRA
Bw Elijah Mwandumbya mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza
sukari cha Manyara Sugar Company Limited kilichopo mkoani Manyara na
kuongeza kuwa takwimu hizo zitawezesha TRA kufuatilia kwa karibu na
kupata takwimu sahihi za kikodi na kuongeza makusanyo ya mapato.
“Tunafahamu kwamba “Molasis” au mali ghafi
inayotokana na zao la miwa baada ya kutengeneza sukari ni bidhaa inayotumika
kutengenezea pombe kali na hivyo takwimu zitatuwezesha kufuatilia wafanyabiashara
wanaonunua bidhaa hiyo na kutengenezea pombe kali ili nasi tukadai kodi
yetu na kodi hiyo ilete tija kwa taifa”, amesema Bw. Mwandumbya
Naye Mkuu wa mkoa wa Manyara Bw. Alexander Mnyeti
amesema mkoa una mkakati wa kuongeza viwanda vingi vikubwa na vidogo
ili viweze kuleta tija kwa mkoa kwa kuongeza ajira na pato la taifa
kwa ujumla.
“Tunataka kuongeza viwanda vingi katika mkoa wetu
ili serikali iweze kupata kodi zaidi na kuongeza mapato kwa ajili ya
maendeleo ya wananchi wetu”, amesema Bw. Mnyeti.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha sukari
cha Manyara Sugar Company Limited, Bw. Pratap Sisudya ameshukuru ujio
wa Kamishna wa kodi za ndani na kuahidi kushirikiana na TRA kuhakikisha
kuwa wanalipa kodi zote kwa wakati pamoja na kutoa takwimu sahihi za
uzalishaji wa kiwanda.
“Ni wajibu wetu kutoa taarifa zahihi kwa TRA pamoja
na kulipakodi stahiki kwa wakati ambapo kwa mwaka 2017/2018 tumelipa
kodi kwa serikali takribani Shilingi bilioni 1”, alisema Bw. Sisudya.
Kiwanda cha Manyara Sugar Company kinazalisha zaidi
ya tani 4,000 za sukari kwa mwaka na kina mashamba ya miwa ekari 1,600
na kutoa ajira za muda kwa watu 350 hadi 400 kwa siku.
Post a Comment