KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUUNDA TAASISI ZA USHAURI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akifafanua jambo kwa
wahandisi washauri (hawapo pichani) wakati wa kongamano la wahandisi
hao la kujadili mafanikio na changamoto katika sekta hiyo.
Baadhi ya wahandisi washauri wakimsikiliza
mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho (hayupo pichani) wakati
wa kongamano la wahandisi hao la kujadili mafanikio na changamoto katika
sekta hiyo.
Baadhi ya wahandisi washauri wakiwa katika
picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho wakati wa kongamano
la wahandisi hao la kujadili mafanikio na changamoto katika sekta hiyo.
Picha na MAELEZO
..........................................................................
Na Grace Semfuko
Maelezo
KATIBU Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Uchukuzi Mhandisi, Dkt.
Leonard Chamuriho amesema kuwa ipo haja kwa Wahandisi washauri nchini kuunda
taasisi ya pamoja ya ushauri ili kuinua taaluma hiyo, ambayo itafanya kazi kwa ufanisi
kwenye sekta ya ujenzi.
Chamuriho amesema,”Iidadi
ya taasisi za uhandisi ushauri zilizosajiliwa nchini ni 413, zenye wahandisi wa
ndani 213 ikiwa ni sawa na wastani wa wahandisi 2 kila taasisi moja hatua
ambayo inatajwa kutokuwa na ufanisi wa kizalendo wa usimamizi wa miradi ya
ndani”
Amesema hayo wakati
akifungua kongamano la siku moja la Wahandisi washauri wa ndani lililoandaliwa
na Bodi ya Ushauri wa Wahandisi- ERB
na kuongeza kuwa, iwapo wahandisi washauri watakuwa na taasisi ya pamoja
itasaidia kuleta ufanisi wa miradi itakayosimamiwa na taasisi hiyo ambayo ni ile iliyojengwa kwa weledi mkubwa.
Naye, Mwenyekiti wa
Bodi ya ERB Mhandisi Profesa Ninatubu
Lema amewataka wadau wa sekta ya uUenzi nchini kutumia wahandisi washauri wa
ndani, kwani wamekuwa wakifanya kazi za ushauri wa miradi mikubwa.Miradi hiyo
ni kama ujenzi wa Reli ya Kisasa ya
Standard Gauge,ujenzi wa barabara za juu za kupishana Fly Overs,majengo makubwa ya kisasa pamoja na miradi mingine.
“Kuna watu wanadhani
tunawategemea sana Wahandisi wa Kigeni,Hapana! Watanzania tunaweza,ndugu zangu
tuwatumie wahandisi washauri wa ndani kwani wanaweza kufanya makubwa,majengo
mengi makubwa ya hapa nchini yamejengwa na yanaendeiea kujemgwa na Wahandisi wa
ndani,tuwaamini,tuwape kazi” amesema Profesa Lema.
Akisisitiza jambo
hilo,Profesa Lema amesema kuwa kutokana
na kazi nzuri zinazofanywa na ERB hivi sasa imerahisisha kutoka eneo moja kwenda lingine. Hii imetokana
na juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , yenye usimamizi
madhubuti wa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli na kuwa na miundombinu mizuri
ya barabara , ambapo zamani ilikuwa vigumu kuifikia Tanzania yote kwa muda
mfupi.
Akifafanua kuhusu
kongamano hilo Lema amesema, kuwa kongamano
hilo la Wahandisi washauri linafanyika Jijini Dar Es Salaam ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa ERB. Bodi hiyo ya ushauri wa
wahandisi ilianzishwa na Serikali ya
Jamhuri Muungano wa Tanzania Oktoba 10 mwaka 1968 na mpaka sasa imeshafanya
ushauri wa miradi mingi nchini.
Kwa upande wake Kaimu
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandishi ERB Mhandisi Patrick Barozi amesema ili
kukidhi Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda,wahandisi
wanahitaji kufanya kazi kwa uzalendo zaidi.
Bodi hiyo ya
Wahandisi ina jumla ya wahandisi waliosajiliwa 22226 elfu kati ya hao wahandisi
Wanawake ni 2200 ambao ni sawa ya asilimia 9.9 ya waandisi wote . Aidha
wahandisi washauri ni 413



Post a Comment