Ads

"SERIKALI YA CCM NIIPENDE KWA LIPI? WALIKATAAKUNITIBIA NILIMWAGIWA TINDIKALI" SIHAMI CHADEMA. KUBENEA.


Na John Luhende 
Mwambawahabari 
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amesema hana mpango wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuwa serikali ili shindwa kumsaidia alipomwagiwa tindikali wakati wa awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu  Jakaya Kikwete.

Amesema sababu za aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara kuhama CHADEMA ni za kipuuzi na kwamba yeye hawezi kufanya kitu kama hicho.

"kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mwita Waitara  kujiunga na CCM  kumekuwa na maneno na wengine wametengeneza  clip zinatembea Polepole anasema Kuna wabunge wengine wa upinzani mmoja wa Chadema Dar es Salaam, sija wahi kuzungumza na mtu yeyote wa CCM kwamba ni nataka kujiunga na Chama Chao. Alisema

Aidha amesema kwa madhara aliyo pitia kwa kumwagiza tindikali serikali ya CCM ilikataakumtibu ingawa  Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Jakaya Kikwete alia hiding mbele ya Umma kuwa angetibiwa lakini baada ya kupelekwa kutibiwa hakutibiwa na Pesa ya serikali.

"Nimefanyiwa Operesheni ya macho maranne nimetibiwa India, Uingereza, na uholanzi sijatibiwa na pesa ya serikali, na sasa hivi nikiwa Mbunge nimeona kwenda kutibiwa  macho nje maratatu lakini sija wahikupelekwa, sasa niipende CCM  kwa lip?!" Alihoji Kubenea

Amesema anafahamu  kazi hii ya kuchafua  watu inafanywa na  baadhi viongozi waliomo ndani ya CHADEMA  kwa maslahi yao na wanafamiana na kuwataka wakafanyekazinyingine.

" Mimi siondoki humu kamakunamtu matatizo tuta rekebisha nikiwa humu humu,  matatizo huwa hatarishi hata kwenye ndoa kunamatatizo nayakinishinda nitaondoka nikimaliza muda wangu na nitaenda kufanya shughulizingine maana mimi ni mwandishi vinginevyo hakuna mtu at aye niondoa nasiondoki"  Amesema

No comments