MAHAKAMA KUU YALITOA KIFUNGONI GAZETI LA MWANAHALISI.
Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imelifungulia gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa na Serikali kutokana na kile kilichodaiwa kuchapisha habari ambazo zipo kinyume na maadili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam, Mkurugenzi wa Mwanahalisi Publisher, Saed Kubenea amesema baada ya kufungiwa gazeti la mwanahalisi walikwenda kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.
Amesema kuwa baada kufungulia kesi hiyo iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja mahakama kuu imeona gazeti la mwanahalisi lilifungiwa kimakosa.
Kubenea ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo amesema kuwa kwa mujibu wa hukumu ya mahakama imeoshenya Waziri hakuwa na sheria katika kulifungia gazeti hilo.
Katika kesi hiyo Mwanahalisi ilisimamiwa na Wakili wawili ambao niJeremia Mtobesya akiongozwa na Wakili wa kujitegemea Dkt. Regemeleza Nshallah.
Katika hatua nyengine amebainisha kuwa wanatarajia kwenda mahakamani kwa ajili ya kumdai fidia waziri aliyelifungia gazeti la mwanahalisi.
Mwaka wa jana gazeti Mwanahalisi lilifungiwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na kile kinachodaiwa kuwa na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.
katika taarifa yake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abassi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema kuwa serikali imechukua uamuzi wa kulifumgia Gazeti hilo kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017, ambapo kwa muda mrefu idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.

Post a Comment