AIRTEL MONEY YAUNGANA NA SERIKALI KURAHISISHA MALIPO KUPITIA MFUMO WA GePG
Mwamba wa habari
Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania imezindua mfumo
wa malipo wa kidijitali kwa huduma za serikali utakaowezesha wateja wa mtandao
huo zaidi ya milioni 10 kufanya malipo ya bili mbalimbali kupitia huduma ya
Airtel Money.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda amesema mfumo huo utatoa
suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa papo kupitia huduma ya Airtel Money.
“Idadi ya wateja wa Airtel Money inakua siku hadi siku na
hivyo kufanikisha moja kati ya malengo ya serikali kuhakikisha kuwa
inafanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kila mahali yaani mjini na
vijijini. Nachukua fursa hii kuwaomba watanzania kutumia mfumo huu kwani ni
salama,” amesema Nchunda.
Naye Mwakilishi wa Mfumo wa Malipo ya Kidijitali wa
Serikali- GePG, Basil Baligumya amesema hadi sasa taasisi za serikali takribani
260 zimejisajili kwenye mfumo huo ikiwemo Halmashauri, Brela, Tanesco, Dawasco.
“Mfumo huo wa serikali kwa ajili ya kulipia huduma zote za
serikali, kumrahisishia mwananchi kulipa kupitia mitandao ya simu, unatengeneza
namna ambayo inafanana katika kulipia huduma zote za serikali kwa taasisi
zilizounganishwa ikiwemo halmashauri, huduma za umeme, maji.
Taasisi taribani
260 zimeingia kwenye mfumo huo, mfano brela tbc b, mfano, ukiingia kwenye menu
ya airtel ndani ya kipindi si kirefu
taasisi zote za umma zitaingia kwenye mfumo huu zinazotoa huduma kwa umma.

Post a Comment