MBUNGE ROSE TWEVE AMBANA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA JUU YA FIDIA ZA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI,
Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiuliza swali la nyongeza kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba juu ya idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa makini kuandika hoja ambazo anajibiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
Na Fredy Mgunda,Dodoma.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa
iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amelibana jeshi la polisi nchini
kupitia kikosi cha usalama barabani kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi
wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali
hizo
Mbunge Rose Tweve mapema hii
leo bungeni aliuliza swali kwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa kutaka
kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na
jeshi hilo.
Akijibu swali la mbunge Rose
Twelve Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba alisema kuwa
jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani limeweza kupunguza
ajali za barabarani kwa asilimia 43 kwa mwaka 2017
Mwigulu alisema kuwa katika
kipindi cha mwaka 2016-2017 kulitokea ajali 9856 ambazo zilisababisha vifo 3256
na majeruhi 2128 ambapo kwa mwaka 2017 kulitokea ajali 5310 na kusababisha vifo
2533 na majeruhi 5355.
Waziri Mwigulu ameongeza kuwa kwa
kipindi cha januari hadi februari 2018 kumetokea ajali 769 na kusababisha vifo
334 na majeruhi 698.
Akiuliza swali la nyongeza
mbunge Rose Tweve alimtaka waziri kutoa idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa
fidia na mwaka 2009 bunge ilipitisha sheria ndogo namba 10 ya bima ya kuwalinda
wahanga wa ajali hizo,sasa mheshimu waziri hawa wenzetu wa TIRA wanaonyesha
wanamapungufu mengi na watanzania wamekuwa wanahanga wakubwa kwenye swala hilo
na kwanini tusianzishe idara maalum ambayo itakuwa inatoa elimu kwa wahanga wa
ajali pindi inapotekea na kujua nini cha kufanya.
Akijibia swali la Nyongeza la
Mbunge Rose Tweve la kuhusu idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia, Waziri
Nchemba amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2018 jumla ya wahanga wa
ajali 1583 wakilipwa
fidia takribani Bilioni 7 kutoka makampuni mbalimbali ya bima.
Katika hatua nyingine Mwigulu Nchemba
amekiri kuwepo kwa matukio ya ajali 1500 yanayosababishwa na uzembe wa madereva
huku serikali ikipanga kuwachukulia hatua madereva wenye tabia hizo.
“Ni kweli serikali itahakikisha
inawachukulia hatua madereva wazembe ikiwemo kuwanyang’anya leseni ili
kupunguza idadi ya madereva ambao wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza
kuepkukika” alisema Mwigulu nchemba.
Post a Comment