WAZAZI MBURAHATI CCM ,WAENDELEA KUFANYA KAZI ZA KIJAMII,KING MLANGA ASEMA NIZOEZI ENDELEVU
Na.John Luhende
Mwamba wa habari
Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ubungo katika kuadhimisha wiki ya wazazi wameendelea kufanya kazi za kujitolea katika mjamii ikiwemo kupanda miti na kufanya usafi katika taasisi za umma.
Akizungumza katika zoezi la kupanda miti lililofanyika katika zahanati ya Mburahati kata Mburahati Katibu wa Elimu ,Mazingira na Uhamasishaji wa jumuiya hiyo King Rashid Mlanga, amesema jumuiya hiyo imeamua kufanya usafi na uhifadhi wa mazingira kwakuwa ilikufanya mazingira kuwa safi ili kujikinga na magonjwa yanayo sababishwa na uchafu.
Amesema
katika kuunga mkono agizo la Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassani ,na kamein ya usafi niliyo anzishwa na Rais Dr John Pombe
Maufuli alipo wataka watanzania kufanya
usafi wa Mazingira ili nchinzima ilikupunguza uharibifu
na uchafu wa mazingira.
‘’Katika
kutekeleza yetu ya CCM nilazima kila kiongozi awajibike katika nafasi yake na nataka niwaagize viongozi wote wa EMAU
kila mmoja awajibike katika nafasi yake katika kutoa huduma kwa wananchi’’
Alisema Mlanga
Ameongeza
kuwa,Jukumu la msingi la viongozi wa CCM nipamoja na kusikiliza kero za
wananchi na moja ya kero kubwa ni Mazingira na kwamba kufanya usafi katika
Zahanati hiyo ni kutekeleza maagizo ya viongozi wa juu katika Chama na Serikali.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya
wazazi Wilaya ya Ubungo Eva Manembe, amewataka wazazi kuendelea kuhamasisha wazazi kwa
Malezi kwa vijana wao ili kupunguza tatizo la Dawa za kulevya .
Hata
hivyo mwenyekiti wa jumiya hiyo Kata ya
Mburahati John Mapunda ameiomba
serikali kujenga majengo ya wodi za wazi Mama na mtoto katika zahati hiyo ilikupunguza usumbufu wanaupata akina mama.
,,Mkurugenzi
wetu ni msikivu na anatujali nimuombe tu atusaidie atujengee wodi ili mama zetu wasihangaike’’.Alisema Mapunda.
Naye Mganga
mfawidhi wa Zahanati hiyo Laura Mbando ameshukuru ujio wa wana CCM kufanya
usafi katka eneo hilo na kusema kuwa kumekuwa na msongamano wa watu katika
eneo la Mburahati jambo ambalo
linasababisha uchafunzi wa mazingira na
tishio la magonjwa ya kuambukiza.
Post a Comment