WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’.
NA MWANDISHI WETU – ZANZIBAR
ZANZIBAR
itakuwa mwenyeji wa michezo ya watu wenye ulemavu wa akili inayotarajia
kuanza Desemba 7-10 katika uwanja wa Amaan ulioko Zanzibar.
Katika
harakati za kuelekea mashindano hayo ya Taifa yanayotarajia wanamichezo
525 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakiwemo wenyeji.
Michezo
hiyo ya walemavu itashirikisha michezo ya soka, Wavu na Riadha ambayo
itachezwa katika mfumo wa michezo jumuishi ambayo inashirikisha watu
wenye ulemavu wa akili na wasio na matatizo hayo, lengo likiwa ni
kuachana na unyanyapaa ndio maana wanacheza timu moja.
Mfano kwenye timu moja ya soka, wachezaji saba ni wazima na wanne wanakuwa ni walemavu wa akili.
Baada
ya michezo hiyo ya Zanzibar, Tanzania inatarajia kushiriki michezo ya
dunia inayotarajia kufanyika mwakani nchini Abu Dhabi.
SOT nini watafanya?
Kuelekea
katika michezo hiyo Kamati ya Olimpiki Maalum (SOT) ambayo ndiyo
wasimamizi imejipanga na matukio kadhaa kuelekea michezo hiyo kwa kuanza
kuwapokea na kuwapeleka Zanzibar kwenye michezo hiyo.
SOT
watapokea wanamichezo 450 kutoka mikoa mbalimbali wakiwa na makocha wao
75 ambao wanatarajia kuwapokea Desemba 5 na kuwapa mapumziko ya saa
kadhaa ambayo yatakuwa katika Jeshi la Wokovu Kurasini kabla ya saa
chache kuelekea bandarini kwa ajili ya safari ya Zanzibar kwa meli ya
Sealink.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa SOT, Dk. Juma Mwanandi Mwankemwa Desemba 6,
wanamichezo hao pamoja na makocha wao watatembelea vivutio vya utalii
vilivyoko Zanzibar huku na kugaiwa vifaa vya ushiriki Desemba 7 itakuwa
ni siku michezo hiyo kuanza.
Dk.
Mwankemwa anasema michezo hiyo itafunguliwa Desemba 7, kwenye uwanja wa
Amaan, Zanzibar ambako kabla ya michezo hiyo kuna baadhi ya taratibu
ambazo wameziweka bayana kati yao na wenyeji Zanzibar ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya mashindano hayo.
Anasema
mikoa yote imeshapata taarifa za ushiriki wa michezo hiyo ambayo
itagharamiwa na SOT kuanzia Jeshi la Wokovu hadi mwisho wa mashindano
hayo.
Makamu
Mwenyekiti wa SOT, Mohamed Mwinyi Ramadhani anasema wamefanikisha suala
la malazi kwa wanamichezo wote ambako wanamichezo watalala katika shule
za Mwanakwerekwe C na Urafiki .
Ramadhani
anasema watafanya ukarabati kidogo katika shule hizo wiki moja kabla ya
michezo hiyo ndio watafanya marekebisho hayo ili wanafunzi walale
katika maeneo salama.
Anasema kutakuwa na mabasi matano na Canter moja ambako pia kutakuwa na gari la wagonjwa (Ambulance).
Michezo hiyo iitangaze Zanzibar
Mjumbe
wa Bodi ya Olimpiki Maalum Zanzibar, Saada Hamad Ali anapendekeza
kwamba ujio wa michezo hiyo kisiwani humo ni kukitangaza kisiwa hicho
kiutalii kwa kuongeza watalii zaidi kwa sababu Zanzibar kuna maeneo ya
kihistoria.
SOT wakutana na wenyeji Zanzibar Novemba 7
Wajumbe
watano wa Bodi ya SOT ilikutana kwa mikutano kadhaa na kamati ya
maandalizi ya Zanzibar, mkutano wa kwanza ulifanyika kati ya Kamati hizo
mbili na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud ambaye
ndiye mwenyeji wa michezo hiyo.
Katika
mazungumzo hayo, Mahmoud anasema yapo masuala ambayo wameshayazungumza
na Kamati ya Zanzibar kwa lengo la kuweka sawa michezo hiyo kufanyika
kwa ufanisi.
Mahmoud
anasema anakubaliana na mfumo wa kuunda kundi la Wassap kwa ajili ya
kufikia mafanikio ya michezo hiyo ambayo itakuwa na idadi kubwa ya
washiriki .
Rais Shein mgeni rasmi katika ufunguzi
Katika
mikakati ya kufanikisha michezo hiyo, Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi utakaofanyika Desemba 7 huku kukiwa na matukio mengine
mbalimbali.
Samia Suluhu mgeni rasmi ufungaji
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Desemba 10 anatarajia kufunga michezo hiyo.
Kamati za maandalizi zaundwa BTMZ
Baada
ya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kikao kingine kilifanyika
katika ofisi za Baraza la Michezo Zanzbar (BTMZ) lililoko chini ya
Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, kikao kilichoongozwa na
Katibu Mkuu wa baraza hilo, Khamis Ali Mzee.
Katika
mkutano huo, ziliundwa kamati saba kwa ajili ya kufanikisha michezo
hiyo zikiwemo Ufundi, Mapokezi, Chakula, Afya, Ulinzi na Usalama,
usafiri na Habari na Uenezi.
Kamati
ya Ufundi inaundwa na Tifli Mustafa Nahoda, Mkurugenzi wa SOT Charles
Ray, Omar Bakar na Lightess Mbilla huku Kamati ya Mapokezi inaundwa na
wajumbe Abdallah Mohamed Ali, Mussa Abdul Rabi, Abdallah Hassan Ali na
Salama Mohamed Ame huku Kamati ya Chakula inaundwa na Saada Hamad Ali,
Kondo Ramadhani Karume, Amour Ali Khamis na Nassor Idrissa.
Kamati
ya Afya inaundwa na Dk. Khatib Juma Bai, Dk Juma Mwanandi Mwankemwa,
Kamati ya Ulinzi na Usalama inaundwa na Seif Haji Ame, Haidar Madowea na
Zainab Omar Mtuli, Kamati ya Usafiri inaundwa na Abdul Wahab Dau, Juma
Ali Juma na Usi Heri Chimbeni.
Kamati ya Habari na Uenezi inaundwa na Eshe Hamad Ali, Mohamed Mwinyi, Makuburi Ally, Salum Vuai na Abubakar Khatib Haji .
Ngoma ya Kibati kusindikiza michezo
Michezo hiyo itakayoshirikisha wadau mbalimbali wa michezo, itasindikizwa na Ngoma ya asili yak visiwani, Kibati.
Post a Comment