CUF yawaomba radhi wanachama wake wa jimbo la Kinondoni.
Mwambawahabari

Chama cha Wananchi (CUF) kimewaomba
radhi wapiga kura wa Jimbo la Kinondoni kufuatia Mbunge wake wa Jimbo
hilo Maulid Mtulia kujiudhuru Ubunge na kujiunga na Chama cha Mapinduzi
(CCM).
Akizungumza na Wanahabari leo jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF,
Abdul Kambaya, amesema chama hicho kinaomba radhi kutokana na
kuwaaminisha wapiga kura kwamba Mtulia ni mtu makini mwenye uwezo wa
kusimamia Sera za CUF na maendeleo ya Kinondoni.
“CUF haikutarajia kuingia kwenye
uchaguzi mdogo kwa jimbo la Kinondoni kabla ya uchaguzi wa 2020 labda
kama ingetokea kifo. Tunaomba radhi kwa kuwa tunaamini katika kurudia
uchaguzi zitatumika fedha za umma wakati kwa hali tuliyo nayo fedha hizo
zingeweza kuelekezwa kwenye shughuli za miradi ya maendeleo. Sababu za
Mtulia kujiudhuru ni za msingi kwake lakini kwa upande wetu tunaziona
hazina mashiko,” amesema
Kambaya amesema CUF inajiandaa
kushiriki katika uchaguzi wa marudio ili kutetea jimbo la Kinondoni na
kwamba itahakikisha inateua Mgombea makini na muadilifu atakayeleta
ushindi kwa chama hicho.
Post a Comment