Ads

WADAU WA JUKWAA LA KILIMO WAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUONGEZEWA KWA MAAFISA UGANI KATIKA HALMASHAURI NCHINI.


 Mkurugenzi wa  Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo, (ANSAF)Audax Rukonge akizungumza na Waandishi wa habari hawapo picha ni  wakati wa MKutano wa wadau wa Killimo kujadilia masuala mbali mbali kuhusu Kilimo.
Mwambawahabari 
Serikali imeshauriwa kusambaza  Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ili waweza kumsaidia  Mkulima  aweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi na kuongeza mavuno.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo (ANSAF),Audax Rukonge   wakati wa Mkutano uliowashirikisha wadau mbali mbali wa Kilimo kujadili kuhusu huduma za Ugani kwa kulima ili ziendane na shughuli ya Viwanda hapa nchini.

Amesema  kitendo cha sasa cha kumtumia Afisa Mgani mmoja katika Kijiji kimoja  ni kitendo ambacho hakiwezekani katika kumsaidia Mkulima.
“Afisa Ugani katika Kijini Kimoja, ni kitu hakiwezekani,maana leo tunasema tuna kijiji kimoja na kesho tukawa na vijiji ishirini hivyo itashindikana kwa afisa Ugani huyu kufanya kazi kwenye vijiji vyote, ni vema serikali ikaliangalia hili”Amesema Rukonge.

Amesema  kutokana na hali ilivyo ya uchache wa Maafisa Ugani kunahaja ya sekta binafsi kuwekeza kwenye utoaji wa Huduma ya  Ugani kwa Wakulima  ili iwe rahisi kwa Mkulima kusaidika.

“Sasa kuna haja sekta binafsi kuwekeza kwenye kutoa huduma ya Ugani  kwa wakulima ili waweze kulipia kwa kiasi husika cha fedha ,kwa mfano kwa wale wakulima wafugaji kama Ngome anaumwa Nyumbani hanahaja ya kumsubili  aje Afisa Ugani bali anamtafuta Afisa ugani  wa Sekta Binafsi anampa hela anamsadia “Amesema Rukonge.

Kwa Upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine (SUA)Dk Sizya Lugeye ambaye ni  miongoni wa wadau hao  katika mkutano huo, ameishauri  serikali Kuhakikisha wanawaongezea nguvu maafisa Ugani waliopo ikiwemo kuwapata fedha pamoja vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanizi zaidi katika kuwahudumia wakulima.

No comments