TAARIFA YA MEYA WA JIJI LA DAR ISAYA MWITA AKIKANUSHA KUHUSU KUDAIWA KUTAKA KUHAMA CHAMA CHA CHADEMA
Ndugu
waandishi wa habari: Nimeshikwa na mshtuko, simanzi baada ya kusambaa
kwa taarifa ambazo naweza kusema kuwa ni za uzushi kwamba
ninampango wa kujiondoa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema. naomba taarifa hizo zipuuzwe manahazina ukweli wowote na kwamba
zinampango wa kunichafua mimi pamoja na Chama Changu.
Ndugu
wandishi wa habari : Napenda ieleweke kuwa sijawahi kudhani wala
kufikiria kuhama Chadema na kwenda kwenye chama chochote kile cha siasa.
Chadema ni chama ambacho nimetoka nacho mbali tangu mwaka 2004 hadi
leo, nimejenga chama kwa gaharama zangu mwenyewe.
Ndugu waandishi
wa habari: Leo nimekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam kupitia Chama
Changu cha Chadema,natambua kuwa chama kimeniheshimu sana kwa kunipa
nafasi hii hivyo sina sababu ya kuondoka kwani ninania ya kuwatumikia
Wananchi ambao wameniamini na wamenichagua kwa mapenzi yao wakiamini
kuwa nitawaletea Maendeleo nikiwa ndani ya Chama Cha Chadema.
.Nafahamu
tuhuma hizi zinatokana na aina ya utendaji wangu katika Jiji la Dar es
Salaam kwani nimekuwa nikifanya kazi badala ya kupambana na serikali
pale ambapo watu wanaamini kuwa mambo hayajaenda sawa.
Ndugu
waandishi wa habari: Kukaa kwangu kimya huku ,kutokufanya siasa za
kiharakati ndani ya jiji la Dar es Salaam haimanishi kwamba nipo upande
wowote ama kukihujumu chama changu. Ila huu ni mfumo ambao nimeuchagua
na kujijengea kwa ajili ya kuwatumikia wananchi nasio kufanya harakati
za kisiasa kwakuwa nina nia ya kufanya maendeleo ndani ya jiji la Dar
es Salaam.
Post a Comment