Ads

SIMBA KUJIFICHA TANGA






Wekundu wa Msimbazi Simba Sport Klabu wameamua kuhamishia kambi yao mjini Sumbawanga Mkoani Tanga kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ya ligi kuu Tanzania Bara.

Simba ambayo ilikuwa Katavi ambapo ilicheza mechi ya kirafiki na kutoka sare ya 0-0, sasa imehamia mjini Sumbawanga na kuanzisha kambi ili kujiweka sawa na michezoijayo.

Kambi ya Simba mjini Sumbawanga itaendelea hadi Jumamosi itakapocheza na Rukwa FC ikiwa ni sehemu ya mechi nyingine ya kirafiki walizopanga kucheza.

Baada ya mechi hiyo, Simba itafunga safari kurejea Mbeya kufanya maandalizi yake ya mwisho dhidi ya Prisons ya Mbeya.
Simba itaanza kujifua leo alasiri kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, uwanja ambao utatumika katika mechi yao dhidi ya Rukwa FC.

No comments