TAMBE AJIDHATITI KUKABILIANA NA SIMBA
Tambwe ndiye mshambuliaji aliyewafunga mabao mengi dhidi ya Simba katika kikosi cha sasa cha Yanga.
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina ameiambia tovuti ya Mwanaspoti.co.tz kuwa Tambwe amepona majeraha yake na sasa yuko sawa anasubiri kuingia kambini na wenzake.
Lwandamina alisema mshambuliaji huyo mkongwe ataongozana na kiungo na nahodha msaidizi wa timu hiyo Thabani Kamusoko kuingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.
Alisema bado hajajua kama Tambwe atacheza mchezo huo, lakini endapo atamuona yuko tayari hatasita kumpa nafasi kutokana na mshambuliaji huyo.
"Nimeambiwa Tambwe naye amepona kabisa na ametaka kuingia kambini kwetu ni taarifa njema ambazo kila mmoja angependa kusikia ni mchezaji anayependa kufanya kazi,"alisema Lwandamina.
"Tutakutana naye kambini nafikiri atakuja pamoja na Kamusoko ambaye naye ametuambia ataingia kambini baada ya kumaliza matibabu yake salama."
Post a Comment