TAKWIMU DODOMA KINARA WA MIMBA ZA UTOTONI
Mwambawahabari
Na Anthony Ishengoma- Dodoma
Takwimu zinaonyesha kuwa Mkoa wa
Dodoma ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mimba na ndoa za utotoni
ambapo asilimia ya wasichana wenye miaka kati ya 20 -22 walioolewa kabla
ya kufikia umri wa miaka 18 kwa mkoa wa Dodoma ni asilimia 51
ukilinganisha na asilimia 37 ya kitaifa.
Hayo yamesemwa na Mbuge Viti
Maalum Mkoa wa Dodoma Bi. Tafma Touwfiq wakati uzinduzi wa maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoanza leo Mkoani Dodoma.
Akiongea katika uzinduzi huo
mjini Dodoma Mbunge huyo amesema kwa takwimu hizi maana yake ni kwamba
kati ya watoto 100, watoto 51 wanaoolewa kabla ya kufikia miaka 18.
Ameongeza kuwa watoto wanaozaa
wakiwa na umri mdogo ni asilimia 39 akizitaja taakwimu hizi kuwa
zinaonyesha tunahitaji kuongeza jitihada na kuwekeza Zaidi katika
mikakati yetu ya kumuwezesha na kumuendeleza mtoto wa kike.
Bi. Tafma amewambia wadau wa
maendeleo ya mtoto wa kike katika mkoa wa Dodoma kuwa Mkoa umezinduwa
kampeni ya kupambana na ndoa na mimba za utotoni na kampeni hii ni kubwa
na itaendelea hadi tutakapofikia malengo ya kumkomboa mtoto wa kike na
kumuweka katika mazingira salama ya kumuwezesha kufikia ndoto zake.
Ili kuonesha mkakati wa
kupambana na ndoa za utotoni mkoani Dodoma Mbunge huyo amesema mkakati
unaotumiwa kwasasa ni ule ujalikanao kama magauni manne akiyataja
magauni hayoa kuwa gaunai la kwanza ni kuhimiza mtoto wa kike kuwa ndani
ya sale ya shule, gauni la pili ni nilile la kuhitimu masomo na la tatu
ni gauni la harusi na lakutiza ndoto ni gauni wakati wa ujauzito mtoto
wa kike akiwa ametimiza ndoto zake.
Maadhimisho hayo yanaendelea
mjini Dodoma katika ngazi ya mkoa na kaulimbiu ya mwaka huu inasema;
“Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa Watoto”.
Post a Comment