TFS KUTOA MITI LAKI TANO YA MATUNDA NA MAJI KWA MKOA WA TABORA
Mwambawahabari
Na Tiganya Vincent, RS- Tabora
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri anatarajia kupokea miche laki tano
ya matunda na miti maji kutoka kwa Wakala wa huduma za Mistu Tanzania
(TFS) kwa ajili ya kupanda katika Taasisi mbalimbali mkoani humo.
Hatua
hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za viongozi wa Mkoa wa Tabora na
wadau mbalimbali wa kampeni za upandaji miti zinaendelea katika maeneo
mbalimbali.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Bw. Mwanri kwenye mkutano na Maafisa Elimu Kata Manispaa ya
Tabora alipokuwa akiwaagiza kuhakikisha wanawahimiza walimu wa shule
zote kuendelea kusimamia zoezi la umwagiliaji wa miti iliyopandwa katika
shule mbalimbali hata wakati wa likizo.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa aliongea na Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Huduma ya Mistu Tanzania Profesa Dos Santos Silayo na kukubali kutoa
kiasi hicho cha miti ili kuongeze nguvu katika juhudi za wadau
mbalimbali mkoani humo.
Alisema
kuwa ni vema walimu wakatumia kipindi hiki wakati wakigonja miche hiyo
kuwasili kuendelea na maandalizi ya kutenga maeneo ya upandaji wa miti hiyo kwa kuanda mashimo, chupa, fito, kamba na mbolea.
Bw.
Mwanri alisema kuwa miti ya matunda mingi itapandwa katika Taasisi kama
vile Hospitali , Vyuo na Shule kwa ajili ya kutunza mazingira na
matunda kwa ajili ya jamii iliyopo katika eneo husika.
Kwa
upande wa miti iliyokwishwa pandwa Mkuu huyo Mkoa amewaagiza Maafisa
Elimu hao wa Kata kuhakikisha wanawahimiza Walimu kuwasimamia wanafunzi
ili waweze kumwagiliaji miti hiyo maji walau mara mbili kwa wiki wakati
wa kipindi chote cha likizo.
Aidha
, Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabara
Mkoa wa tabora kusaidia kusimamia usalama wa wanafunzi kuvuka barabara
wakati siku ambazo zitatengwa na Manispaa ya Tabora kuwa ndio za
umwagiliaji.
Naye
Kaimu Afisa Elimu wa Manispaa ya Tabora Gaudencia Kafu alisema kuwa
zoezi la umwagiliaji litakuwa likifanyika mara mbili kwa wiki kwa siku
ya Jumatatu na Alhimisi ili kuhakikisha miti hiyo inaendelea kukua.
Alisema kuwa anatarajia kutoa maelekezo hayo kwa Shule zote za Manispaa kabla ya wnafunzi hao hawajafunga siku ya Ijumaa.
Post a Comment