Elimu zaidi inahitajika kuhifadhi mazingira nchini
Mwambawahabari
WAKATI Mataifa mbalimbali
yanaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani yanayofikia kilele chake hapo
Juni 5, 2017, takriban hekta 372,000 za misitu hupotea kila mwaka nchini
Tanzania kutokana na shughuli mbalimbali. Mwandishi Beatrice Lyimo wa
Idara ya Habari – MAELEZO anaelezea zaidi. Kwa miaka mingi siku
ya Mazingira duniani imekuwa ikiadhimishwa kwa Wadau katika nchi
mbalimbali kuchukua hatua chanya zinazohusu mazingira. Siku hii pia
imekuwa ni sehemu ya kampeni ya utoaji elimu juu ya maswala
yanayojitokeza kuhusiana na mazingira.
Kauli mbiu katika maadhimisho ya
mwaka huu inasema “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira”
ikihamasisha jamii kuwa na urafiki endelevu na mazingira asilia ambapo
kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa
mazingira asilia na kuhamasishana ili kuyatunza na kuyahifadhi.
Tanzania kama ilivyo kwa nchi
nyingi Barani Afrika na duniani kwa ujumla imeendelea kuathirika kwa
kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli
mbalimbali zikiwemo za kilimo, ufugaji, ujenzi n.k Mara baada ya
kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu aliagiza
kutofanyika kwa maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika ambayo yalizoeleka na
badala yake Watanzania waadhimishe siku hiyo kwa kufanya usafi. Mtazamo
wa wengi kuhusiana na maelekezo ya Dkt. Magufuli ulilenga zaidi katika
kubana matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Pamoja na mtazamo huo Mhe. Rais
aliona mbali zaidi, kwani usafi wa mazingira unasaidia kudhibiti
milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu, ambayo yanaigharibu
Serikali fedha nyingi zaidi ya zile ambazo zingetumika katika
kufanikisha maadhimisho hayo. Hivyo uamuzi alioutoa Mhe. Rais
utakumbukwa zaidi wakati huu ambapo nchi mbalimbali zinaadhimisha Siku
ya Mazingira Duniani.
\Siku hii inatutaka tutoke nje
tuone mazingira yetu yalivyo, tuone thamani yake na tupaze sauti ya
kuulinda ulimwengu tunamoishi.Inakadiriwa takribani hekta 372,000 za
misitu hupotea kila mwaka nchini kutokana na shughuli za kilimo na
ufugaji kwa njia zisizo endelevu. Uharibifu huu wa misitu unachangia pia
kukosekana kwa mvua, kukauka kwa mito, mabwawa na uoto wa asili.
Akizungumza katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani mwaka jana Makamu wa Rais, Mama
Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kazi ya kuhamasisha na kuelimisha
jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira inahitaji ushirikiano wa
Wadau katika ngazi zote.
Amesema, Serikali inahitaji ushirkiano mkubwa kutoka kwa wananchi, Vyombo vya Vabari, Taasisi na Asasi za Kiraia katika kutekeleza kikamilifu Sheria na Kanuni za uhifadhi wa mazingira nchini ili kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira. Aidha, Makamu wa Rais alizitaka Mamlaka katika ngazi mbalimbali ziwe na Mipango bora ya ardhi, mikakati ya uhifadhi wa vyanzo vya maji, pamoja na udhibiti wa uvunaji holela wa misitu na ufugaji usio endelevu.

Mama Samia pia alizitaka Wizara
na Taasisi zote za Serikali na zisizo za Kiserikali kuendelea kutoa
elimu juu umuhimu wa kutunza mazingira na faida zinazopatikana ili
Wananchi waunge mkono jitihada zinazofanywa katika kulinda na kuhifandhi
mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
“Usafi wa mazingira uhusishe kila mtu kuhakikisha taka zinakusanywa na zinatupwa katika maeneo yaliyotengwa na tupande miti mingi wakati wa msimu wa mvua ili tujihami na kuenea kwa hali ya jangwa na mabadiliko ya tabianchi” alisema Mhe. Samia.
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka 2017/18, Waziri wa Nchi (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema kuwa uchumi wa Tanzania unategemea kwa kiasi kikubwa maliasili zilizopo ikiwemo ardhi, maji, misitu na hewa safi.
Alisema, maliasili zilizopo zinahitajika kwa matumizi ya vizazi vilivyopo na vijavyo, hivyo uwepo wake hutegemea zaidi uhifadhi wa rasilimali hizo na matumizi katika jamii inayotuzunguka.
Aidha, Waziri Makamba alibainisha baadhi ya Changamoto iliyopo kwa sasa ni pamoja na uelewa mdogo wa jamii kuhusu uhifadhi ya mazingira na uwepo wa mabadiliko ya tabianchi. Hivyo juhudi kubwa inahitajika zaidi katika kutoa elimu kuhusiana na mazingira.Kwa mujibu wa Waziri Makamba, Serikali imeanisha programu mbalimbali za uhifadhi mazingira kwa kutengeneza, kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa mipango na mikakati ya Kitaifa ya hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini katika ngazi mbalimbali za utawala.

“Katika mwaka wa fedha 2016/17
Serikali iliwahimiza viongozi na watendaji katika Sektretarieti za
Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekta zote Tanzania Bara
kutenga fedha na kutekeleza na kutolea taarifa mikakati na mipango ya
hifadhi na usimamizi wa mazingira” alisema Mhe. Makamba.
Aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa
Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais
TAMISEMI iliandaa Mkakati wa Taifa wa Kupanda na Kutunza Miti
utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2016 hadi 2021) ambapo
mkakati huo unaelekeza katika kila kijiji, kitongoji, mtaa na kaya .
Amesema, Mkakati huo umezingatia
kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika mikakati na kampeni
zilizopita, ikiwemo motisha na ushiriki wa sekta binafsi katika biashara
ya misitu ambapo baadhi ya mikoa imeanza utekelezaji wa mkakati huo kwa
kupanda miti kwenye maeneo yao.
Tarehe 5 Juni kila mwaka Tanzania
tunaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira
Duniani, ambapo kampeni mbalimbali huandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha
jamii kujenga uelewa wa masuala yahusuyo mazingira kuchukua hatua
stahiki za kuhifadhi na kulinda mazingira.
Post a Comment