WAZIRI KAIRUKI AZINDUZA MAFUNZO UONGOZI KWA MAOFISA WA POLISI.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora
Mhe.Angelah Kairuki akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Ernest Mangu wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa
Maofisa wa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma.Mafunzo hayo yanaendeshwa na
Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini
Finland.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya
nchi Balozi Simba Yahaya
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza wakati wa
Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa Jeshi la
Polisi Mjini Dodoma.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa
kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah
Kairuki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph
Semboja.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora
Mhe.Angelah Kairuki akizindua Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa
wa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi
kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu na kushoto ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi
ya Uongozi Prof. Joseph Semboja.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora
Mhe.Angelah Kairuki (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.
Mwigulu Nchemba (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest
Mangu wakionyesha Vitabu vyenye Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa
Maofisa wa Jeshi la Polisi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa
kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland mjini Dodoma
leo.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika
Uongozi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora
Mhe.Angelah Kairuki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu
Nchemba na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa
wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na
Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini
Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika
Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa “Post-Graduate Diploma in
Leadership”
Baadhi
ya Maofisa wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi
yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto
cha nchini Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa
Polisi katika Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa
“Post-Graduate Diploma in Leadership”.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la
Polisi)
Post a Comment