BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM WILAYA YA KUSINI UNGUJA MAREHEMU HAMDANI.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MJUMBE wa Kamati kuu ya CCM,
Balozi Seif Ali Idd ameongoza mamia ya wanachama wa Chama na Wananchi
kwa ujumla katika mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini
Unguja Marehemu Hamdani Haji Machano aliyefariki ghafla jana kwa maradhi
ya baridi.
Maziko hayo yamefanyika katika
kijiji cha Donge Shehia ya Mtambile Mkoa wa Kaskazini Unguja, na
kuudhuriwa na wananchi pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu,
Halmashauri kuu za CCM, Wenyeviti , Makatibu wa Mikoa na Wilaya, Wakuu
wa Mikoa na Wilaya za Zanzibar pamoja na Wajumbe wa NEC.
Akizungumza mara baada ya maziko
hayo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdalla Juma Saadalla
“Mabodi ” alisema Chama hicho kimepokea kwa mshituko na masikitiko
makubwa taarifa ya kifo cha Mtendaji huyo na kuwaomba wanafamilia, ndugu
na jamaa kuwa na subira katika kipindi hiki cha msiba.
Ameeleza kwamba marehemu Hamdani
alikuwa ni Kiongozi mwadilifu na mchapakazi na aliyekuwa akijitolea
kufanya kazi kwa bidii huku akisimamia kwa dhati maslahi ya Chama hicho.
Dkt.Mabodi alifafanua kwamba
kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na marehemu huyo wakati wa
Utumishi wake, CCM itaendelea kuenzi juhudi hizo kwa kusimamia mamlaka
za kiutendaji ndani ya chama na serikali ili ziendelee kutenda haki kwa
wananchi wote.
“Tumepokea kwa mshituko mkubwa
kifo cha Mtendaji mwenzetu na hili ni pengo kubwa linalotakiwa kuzibwa
na umoja wetu katika na kukitumikia chama chetu kwa uzalendo ili
kishinde kila uchaguzi na kuendelea kuongoza dola kusimamia yote mazuri
yaliyoachwa na Marehemu Hamdani.
Pia nakumbuka hivi juzi tu katika
ziara zangu tulikuwa pamoka katika Mkoa wake wa kazi tukishauriana
mambo mengi ya Kiutendaji na kisiasa, naomba Mwenyezi Mungu amjaalie
mapumziko mema na yenye kheri na yeye Amin.”, alieleza Dkt.Shein.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu
wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka aliweka bayana kwamba Marehemu
Hamdani alisema kwamba ni kada wa kweli yaliyepigana kuona CCM na
Jumuiya zake zinapiga hatua kubwa kimaendeleo.
Naye Mkaazi wa Shehi ya
Chanjaani, Masoud Haji Choum alisema mbali na Marehemu huyo kuwa na
ushirikiano mzuri na viongozi wa chama na serikali pia alikuwa ni mtu
aliyekuwa akipenda kujumuika na jamii katika masuala mbali mbali ya
kimaendeleo, kijamii na kiuchumi.
Akithibitisha mchango wake
Marehemu huyo katika harakati za kisiasa ndani na nje ya Naibu Katibu
Mkuu Mstaafu, Vuai Ali Vuai Alieleza kwamba Hamdani alikuwa ni mtu
makini na mkweli katika utumishi wake na aliyetamani mabadiliko ya
kimaendeleo katika sehemu yake ya kazi na chama kwa ujumla.
Mara baada ya maziko hayo palisomwa wasifu wa marehemu Hamdani kuwa alizaliwa mwaka 1963, huko Donge.
Amewahi kushika nafasi mbali
mbali za uongozi na utendaji ndani ya chama na jumuiya zake baada ya
kujiunga na CCM mwaka 1987 ambapo mwaka 1988 alikuwa katibu wa UVCCM
Tawi la Donge Mtambile mwaka, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kusini hadi
kufikiwa na mauti alikuwa ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja.
Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Amin.
Post a Comment