KAMPUNI YA AGGREY&CLIFFORD YANG’ARA KIMATAIFA
*Yatambulishwa kwenye orodha ya makampuni bora ya matangazo duniani 2017Taasisi
ya kimataifa ya masuala yanayohusiana na makampuni ya matangazo duniani
ya thenetworkone ya nchini Uingerezaimetoa jarida lake la “The World’s
Leading Independent Agencies”la mwaka 2017 mwishoni mwa wiki hiiambapo
kampuni ya matangazo ya biashara na ushauri wa masoko nchini Tanzania ya
Aggrey&Clifford, imetangazwa katika orodha ya makampuni bora
duniani kutokana na mchango mkubwa inaotoa kukuza sekta hiyo.
Aggrey&Clifford, imechomoza miongoni mwa makampuni 12
duniani, matatupekee ndiyo yakitokea barani Afrika,yanayotoa mchango
mkubwa katika kukuza sekta ya matangazo ya kibiashara na makala yake
kuhusiana na umuhimu wa makampuni ya biashara kufanya ubunifu wa chapa
zake za biashara,kuzilinda na kuziendeleza imechapishwa kwenye jarida
hilo ambalo limeanza kuuzwa nchini Ungereza na pia likipatikana kwa njia
ya mtandao kupitia tovuti ya leadingindependents.com.
Makala hiyo imeeleza kwa kina jinsi makampuni mengi yanayowekeza biashara zake barani Afrika yamekuwa na mtindo wa kunakili chapa za mataifa ya nje ya Afrika na mara nyingi kutumia matangazo ya biashara yaliyotengenezwa kwenye nchi hizo ambayo hayaendi sambamba na mazingira na masoko ya bara la Afrika.

Kupitia makala hiyo makampuni
ya biashara barani Afrika yanashauriwa kuhakikisha yanafanya utafiti wa
masoko na kuyaelewa vizuri badala ya kutumia chapa na matangazo
yaliyotengenezwa kwa kulenga masoko ya sehemu nyingine.Afisa
Mtendaji Mkuu wa Aggrey&Clifford, Rashid Tenga, akiongea kuhusu
mafanikio haya alisema “Tunajivunia kuona kampuni yetu inafanya vizuri
nje ya mipaka ya bara la Afrika katika ngazi ya kidunia, kwa kuingia
katika World’s Leading Independent Agencies na ni moja ya hatua ya
mafanikio katika kipindi cha miaka 8 tangia kampuni ianzishwe. Hatua hii
inadhihirisha kuwa makampuni ya kitanzania na Afrika yanayo fursa ya
kufanya vizuri katika ngazi ya kimataifa kama ambavyo imetokea.”
Tenga alisema Aggrey&Clifford, ambayo inafanya kazi na
makampuni makubwa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki, itaendelea kutoa
huduma bora za matangazo ya biashara na ukuzaji wa chapa za biashara za
kitanzania na kutoa ushauri.
Aggrey&Clifford yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam ikiwa na matawi katika nchi za Uganda (Kampala) na Rwanda (Kigali), mbali na huduma za matangazo ya biashara na ukuzaji chapa inatoa huduma mbalimbali za ushauri na ukuzaji wa huduma za makampuni ya biashara na Mashirika yasio ya kibiashara.

Post a Comment