CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZATATULIWA KWA KIASI KIKUBWA : MAKAMBA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na waandishi
wa Habari hawapo pichani juu ya Mafanikio ya Muungano katika
kuadhimisha miaka 53 ya Muungano. Kulia ni Mhe. Jenista Mhagama Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya Maadhimisho ya
miaka 53 ya Muungano yatakayoadhimishwa katika viwanja vya Jamhuri
Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akifuatilia mazungumzo katika
mkutano wa waandishi wa habari juu maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Baraka
Rajab.
…………
Na; Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa – Dodoma
Waziri wa Nchi anayeshughulia
masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, amesema kuwa
changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa
kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto 3 kwaka
huu 2017, Muungano unaotimiza miaka 53 wiki ijayo.
Waziri Makamba amezungumza hayo
leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari
ulioandaliwa na waratibu wa sherehe za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu na kusimamiwa na Waziri Mwenye
dhamana Mhe Jenista Mhagama.
Mhe. Makamba amezitaja changamoto
zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto unaorahisisha
kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda Bara na kutoka Bara kwenda
Zanzibar na kusema kuwa swala hili linafanyiwa kazi kwa kumalizwa kwa
taratibu za kisheria.
Alisema kuwa changamoto nyingine
inahusu Hisa za Zanzibar kwa iliyokuwa bodi ya safari ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Pamoja na Mapendekezo ya tume ya Pamoja ya fedha.
Awali akizungumzia Muungano huo
unaotimiza miaka 53, Waziri Makamba Alisema kuwa umekuwepo kisheria na
umerasimisha udugu na ushirikiano uliyokuwepo kati ya Bara na
Visiwani.
Mkutano huo wa waandishi wa habari
uliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na
Walemavu umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan
Rugimbana, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Ofisi hizo.
Post a Comment