Ads

WADAU WA KILIMO NDANI NA NJE YA NCHI KUKUTANA SIKU TATU KUJADILI MCHANGO WA KILIMO KATIKA TANZANIA YA VYA WANDA


Ba John Luhende
 mwambawahabari
Tanzania  inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Tatu wadau wa Sera za Kilimo AAPC  utakafanyika  kesho jijini Dae es salaam ambapo Waziri  wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Mhe. Charles Tzeba atakuwa mgenirasm, atakaye zindua taarifa ya Bank ya Dunia kuhusu  hali ya mazingira wezeshi ya biashara Tanzania .

Akizunguza  na waandishi wa Habari Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na Kilimo  ANSAF Bwana Audax  Lukonge amesema mkutano huo pamoja na Mada mbalimbali zitakazojadiliwa  pia watatazama  Mchango wa secta ya  kilimo katika kuhamasisha Viwanda nchini , na zaidi ya washiriki zaidi ya miambili kutoka nchi mbalimbali mbali duniani watashiriki mkutano huo.

Aidha amesema  kuwa mkutano huo pia  unalenga katika kuongeza uelewa miongoni kwa watunga Sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuajia wa Viwanda Tanzania , na washiriki pia watazungumzia kuhusu hatima ya wakulima wadogo na Masoko ya asili katika uchumi wa Viwanda  kwa kuwa kilimo kina nafasi kubwa ya Kuongeza pato la Taifa

No comments