Ads

UWARIDI WAZINDUA WA ANZISHA APP YA KUSOMA RIWAYA MTANDAONI



Na Maria Kaira 
Mwambawahabari
Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI) wakishirikiana na kampuni ya Dau Technology Limited leo hii wamezindua mfumo maalumu wa kuuza,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu,yani mobile phone application iitwayo "UWARIDI APP"ikiwa na lengo la kukuza utamaduni wa watanzania kupenda kusoma riwaya.

Akizungumza na waandishi wa habari Jiji Dar es salaam Katibu Mkuu wa UWARIDI APP Ibrahim Gama amesema kupitia mfumo huo utaweza kuwasaidia na kuwakomboa waandishi wa riwaya hapa nchini kupata malipo yao muafaka kupitia kazi zao.



Pia Gama amesema mfumo huo mpya utawezà kuwatambulisha waandishi hao kwa upana zaidi kwa wasomaji wa riwaya wa ndani na nje ya nchi, ambapo Kupitia mfumo huo serikali itaweza kunufaika na kukusanya Kodi sahihi utokanayo na kazi za riwaya.


"Pamoja na kwamba mpaka sasa kuna app nyingine nyingi hapa nchini UWARID APP ndio pekee ambayo ndani yake msomaji atapata riwaya mchanganyiko kutoka kwa waandishi mbalimbali wakiwemo waandishi nguli ambao riwaya zao zimekuwa adimu sana miongoni mwa wasomaji" amesema

Aidha amesema hadi sasa kuna jumla ya waandishi 20 mchanganyiko walioweza kuweka riwaya zao kwenye App hiyo,Ambapo kila wiki waandishi wa riwaya hizo wataweza kuongezeka .

Abdallah Mura kutoka kampuni ya Dau Technology amesema kupitia app hiyo kazi za wana riwaya hao zitakuwa salama na hazitaweza kunakiliwa wala kuuzwa na mtu yoyote nje ya mfumo wao waluoubuni wenyewe.

Hata hivyo Rais wa (UWARIDI APP) Hussein Tuwa amesema kupitia mfumo huo utaweza kuwarahisishia wasomaji wa riwaya nchini kusoma riwaya wakiwa mahali popote pale kwa kutumia simu zao za mikononi.

2 comments: