Ads

Siku ya Wanawake Duniani: DC Lyaniva aagiza vikundi VICOBA kujisajili

mwambawahabari


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amevitaka vikundi vya VICOBA kujisajili mapema iwezekanavyo ili vikundi hivyo viweze kutambulika na kupata uwezeshaji kiuchumi.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, DC Lyaniva ameeleza kuwa vikundi vya VIKOBA vilivyopo ni takribani 2748 lakini kati ya hivyo vilivyosajiliwa na kutambulika ni 746, hivyo vikundi 2200 havijasajiliwa, hivy0 ni vyema vikasajiliwa haraka iwezekanavyo ili viweze kupata fursa hiyo adhimu ya uwezeshaji kiuchumi.
DC Lyaniva ameeleza kuwa Machi 20 mwaka huu kutakuwa na jukwaa la uwezeshaji wanawake katika uwanja wa Mnazi Mmoja ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu hivyo ni vyema wakajisajili mapema wapate fursa hiyo, pia amewaagiza Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuandaa programju ya mafunzo kwa wanawake ambayo itakuwa na tija ya kuwaelimisha na baadae wataweza kujiajiri, hivyo programu hiyo iwasilishwe kwa Mkuu wa Mkoa ndani ya mwezi mmoja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) Maida Waziri amewataka wanawake nchini kujituma na kuwa wabunifu katika biashara zao jambo litakalo wapelekea kufanikiwa, huku akisisitiza elimu na mtaji siyo chanzo cha kukata tamaa bali kufanya kazi kwa bidii na kutumia taarifa sahihi zitakazo wapelekea kufanukiwa kama ilivyokuwa kwake, ambaye amefikia hatua ya kupewa tuzo na Rais Mstaafu Jakaya Kikwetu kwa kuwa Mkandarasi bora 2011-2015.
Siku ya Wanawake Duniani husherekewa Machi 8 kila mwaka, ambapo kitaifa imesherekewa Mkoani Singida na mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, huku kauli mbiu ikiwa Tanzania ya Viwanda Mwanamke ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi.

No comments