WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUSAIDIANA NA WALIMU KUWAREJESHA WATOTO WALIOTOROKA MADRASA
Na Masanja Mabula –Pemba .
mwambawahabari
WAZAZI na walezi wa watoto kisiwani Pemba wametakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa kuwashajihisha watoto waliotoroka vyuoni kurejea na kuendelea na masomo yao .
Lengo kutaka kurejeshwa madrasa watoto hao ni kuisoma dini yao na kuifahamu ili waweze kukabiliana na changamoto mbali mbali za utandawazi.
Wito huo umetolewa jana na msaidizi mwalimu Mkuu wa madrasatul Rahman iliyopo Chanjamjawiri Gereji chakechake Pemba Ustadhi Suleiman Khamis Mohd alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi .
Ustadhi Mohd amesema, kwa sasa hali imekuwa tofauti na zamani kwani watoto wengi kike na kiume wanapofikia umri wa kuanzia miaka 15 hutoroka vyoni na kushuhulikia zaidi na masomo ya kidunia na wengine kuzurura mitaani na hatimaye hutumbukia katika matendo maovu yakiwemo ulevi na mapenzi katika umri mdogo.
Amesema , bado wazazi hawajawa na muamko kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu ya dini ya kiislamu ambayo imeshushwa hadhi kulinga na wazazi pamoja na watoto kutoipa kipaombele .
Aidha amesema ,licha ya madrasa hiyo kutoa mafunzo ya fani tofauti kwa wanafunzi ikiwemo sira, hadithi za mtukufu mtume Muhammad SAW, lugha ya kiarabu na kiengereza , lakini pia wanatoa mafunzo ya compyuta kwa wanafunzi waliomaliza mashafu ili kuwajenga kitaaluma zaidi ya kupambana na mazingira ya ulimwengu wa leo popote wanapokua.
Ustadh Mohd amefahamisha, licha ya kuwepo kwa juhudi kubwa wanazozichukua kuwasaidia wanafunzi katika madrasa yao lakini bado wanakumbana na changamoto kubwa zinazokwamisha juhudi hizo ikiwemo uhaba wa compyuta na walimu wa lugha ya kiarabu na kiengereza.
Amesema kuwa inafikia hadi compyuta moja kutumiwa na wanafunzi wawili hadi watatu kwa wakati mmoja na kulazimika kuwagawa wanafunzi hao katika vipindi vitatu tofauti hali inayopelekea ugumu kiasi fulani.
Ametoa wito kwa serikali, taasisi na watu binafsi kujitokeza kusaidia madrasa hiyo kwani wapo kwaajili ya Allah SW hivyo kutoa kwaajili ya Allah kuna kheri kubwa huko tuwendako.
Amemalizia kwa kuwataka wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika vikao vya madrasa sambamba na kuchangia ada kwa ajili ya walimu waliojitolea kufanya kazi hiyo ngumu inayohitaji uvumilivu wa hali ya juu ili kuwatia moyo wandelee kufanya kazi.
Post a Comment