DC HAPI AZINDUA KITUO CHA MAFUTA CHA KISASA PORT ACCESS CHA TOTAL,
Na John Luhende
mwambawahabari
Kaim Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe, Ally Hapi amewataka wamiliki wa vituo vya mafuta jijini Dar es salaam kukarabati vituo vyote vinavyo onekana kuwachakavu na na kujengwa kizamani ili kuendana na wakati na kutunza mazingira.
Hapi aliyasema hayo katika uzinduzi wa kituo cha mafuta cha kisasa cha kampuni Total kinachojukana kwajina la Total port access kilichojengwa maeneo ya Sokota Temeke jijini Dar es Salaam, amesema vituo vya mafuta vinahitaji kuwa mazingira bora kutokana na huduma wanayoitoa.
Amesema Total imejikita katika uhifadhi wa mazingira kwa kutengeneza vituo bora vya mafuta tofauti vituo vingine ambavyo havisadifu na majina ya kampuni na kuwaasa kuboresha vituo vyao ili kuendana na mazingira ya kisasa.
Aidha Hapi amewaomba wawekezaji hao kujenga kiwanda cha vilanishi nchini kutokana na kuwepo kwa magari mengi na uhakika wa soko kutoka nchi jirani zinazotumia Bandari ya Dar es salaam
"Nimewaomba wajenge kiwanda nadhani niwakati mwafaka wameonyesha uwezo mkubwa kituo walicho kijenga hapa kina mfumo wa kisasa wa kutunza mazingira hata wakijenga kiwanda wataendelea kutunza mazingira yetu serikali itawapa suport na wao wameniambia wako tayari watalifanyia kazi " alisema Hapi
Katika uzinduzi huo ameomba mafuta lita 10,000 kwa kampuni ya Total kwa ajili ya kutumia katika uchongaji wa barabara za manispaa ya Kinondoni ambapo alikubaliwa kupewa lita hizo.
Amesema kuwa kuna kampuni imejitolea kutoa mitambo ya kufanya kazi hiyo lakini waliomba mafuta nijitegemee kwa kupata mafuta kwa hayo kazi itafanyika.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Total, Tarik Moufaddal amesema wataendelea kuboresha vtuo vyao iliviendane na wakati na na huduma wanayoitoa.
Post a Comment