SERIKALI MUONGOZO WA MATUMIZI YA MIHURI KWA WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI
Na john Luhende
mwambawahabari
Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na wenyeviti wa serika za mitaa serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serika.
akizingumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuli kwa wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka pale watakapo jadiliana tena.
''Hakukuwa na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya na heshima yenu menyeviti lakini kama muhuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili" amesema simbachawene.
Sanjari na hayo Simba chawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu za msingi za kutoa muongozo huo kutokana na matumizi mabaya mihuri kwa wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea kuigawa Adhi bila utaratibu maalumu na kusababisha migogoro mingi ya ardhinchini.
Naye Katibu wa Wenyeviti Mko wa Dar es salaam Mariam Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi.
Pamoja na hayo baadhi ya wenyeviti waliofika katikati kikao hicho wamesema kufutwa kwa muongozo huo kuta wapa ahueni wananchi wao kwakuwa shughuli nyingi za kijamii na za serikali zina hitaji mhuri muda wote hata kama ni sikuku hvyo wanachi wao wangepata usumbufu mkubwa kwakuwa watendaji wa mitaa hawaishi maeneo ya yakazi ispokuwa wenyeviti ndiyo wakazi na wako karibu zaidi na wananchi .
Post a Comment