POLISI KANDA MAALU YA DAR ES SALAAM, YAPIGA MARUFUKU UUZAJI HOLELA WA SILAHA ZA JADI.
Na Maria kaira ,
Mwambawahabari
Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imewaagiza wafanyabiashara wote wanaojihusisha na uuzwaji wa silaha za jadi barabarani kuacha tabia hiyo mara moja na badala yake kutafuta sehemu maalumu ya kufanya biashara hizo.
Hayo yametokana na tabia iliyojengeka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujihusisha na uuza wa siraha kama mapanga, visu, manati na upinde pembezoni mwa barabara hususani kwenye mataa ya kuongezea magari.
Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Kamishna wa polisi kanda Maalum Dar es salaam Saimon Sirro amesema biashara hizo zimekuwa hatarishi kwa usalama wa watu wanaotumia Barabara hizo, pia aliongeza kuwa biashara hizo zimeshamiri sana katika Barabara ya Nyerere Tazara mataa, chang'ombe mataa pamoja na Gerezani mataa .
"Nimepiga marufuku uuzwaji wa bidhaa hizo kwasababu watu wanao husika na uuzaji wa bidhaa hizo wamekuwa sio waaminifu na hutumia fursa hiyo kuwatishia watu wanaokuwa kwenye magari binafsi na magari ya umma na kuanza kuwaibia mali zao mbalimbali kama simu za mikononi, saa, mikoba na laptop, pia " amesema
Aidha kamishna Sirro amesema silaha hizo zinatakiwa kuuzwa kwenye maduka yenye leseni na sio vinginevyo ambapo atakayepatikana akifanya biashara hiyo atachukuliwa hatua za kisheria.
" January 12 katika mataa ya Tazara tulimkamata mtuhumiwa Mgoli Sakalani (39) mgogo mfanyabiashara na mkazi wa Banana akifanya biasha hiyo" amesema
Pia Kamishna Sirro amesema kikosi cha usalama Barabarani kanda maalum ya Dar es salaam ya ukamataji wa makosa barabarani katika kipindi cha January 5 hadi January 12 wamefanikiwa kupata Fedha za tozo sh. Milioni 657,060,000.
Post a Comment