Ads

PICHA TEMESA ,DKT. MGWATU AWATAKA WATENDAJI TEMESA KUEPUKA WAZABUNI WANAOUZA VIPURI NA VILAINISHI KWA BEI ISIYO YA SOKO.

Displaying 1.JPG
Pix 1: Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (aliesimama) akifungua mafunzo elekezi juu ya tozo za matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo kwa watumishi wa TEMESA kutoka mikoa 19.  Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Semfukwe na kulia ni Meneja wa TEMESA Dodoma. Mafunzo hayo ya siku 5 yanafanyika Mkoani Dodoma katika ukumbi wa TBA.
Displaying 2.JPG

Pix 2: Washiriki wa mafunzo elekezi juu ya tozo za matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yanayofanyika Mkoani Dodoma katika ukumbi wa TBA wakisikiliza hotuba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (hayupo pichani). Mafunzo hayo ya siku tano yanashirikisha watumishi wa TEMESA kutoka mikoa 19.

Displaying 3.JPG
Baadhi ya washiriki wa mafunzo elekezi juu ya tozo za matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yanayofanyika mkoani Dodoma katika ukumbi wa TBA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (alieketi katikati) baada ya ufunguzi. Mafunzo hayo ya siku tano yanashirikisha watumishi wa TEMESA kutoka mikoa 19.
Displaying 4.JPG
Mameneja kutoka mikoa 19 yenye vituo vya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (alieketi katikati) baada ya ufunguzi wa mafunzo elekezi juu ya tozo za matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yanayoendelea mkoani Dodoma katika ukumbi wa TBA

Picha zote na Theresia Mwami, TEMESA.

No comments