PICHA : SIHABA NKINGA AKUTANA NA WAZEE WA KOO TANO WILAYANI TARIME
mwambawahabari
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na wazee wa kimila kutoka koo tano mkoani Mara ambapo amewapongeza kwa kazi ya kuelimisha jamii inayowazunguka juu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike na tohara mara mbili kwa watoto wakiume, Katikati ni Mtumishi Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) Bi. Kambibi Kamugisha, kushoto ni Katibu Tawala Tarime Bw. John Marwa na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai.
Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore akiongea na na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.
Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya akiongea na na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alimuomba Katibu Mkuu kuangalia uwezekano wa kuwezeshwa kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila kutoka koo tano za Bukenye,Nyabasi,Bukira,Butimbaru na Buhunyaga leo Mjini Tarime
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watoto wa kike walio katika mradi unaotekelezwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) wa kuwawezesha kijasiriamali watoto waliokimbia vitendo vya ukeketaji.
6- Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) na watoto wakike walio katika mradi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiagana na watoto wa kike walio katika mpango wa kuwezeshwa kijasiriamali na Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF)
PICHA NA HASSAN SILAYO
Post a Comment