MASAUNI APIGA MARUFUKU JESHI LA ZIMAMOTO NA UHAMIAJIA KUSHONA SARE URAIANI, AAGIZA ZISHONWE NA MAGEREZA.
mwambawahabari
Na John Luhende
mwambawahabari
NAIBU waziri mambo ya Ndani Hamadi masauni amelitaka jeshi la zimamoto na Uhamiaji kutoshona sare zao za uraiani badala yake wakashone katika jeshi la Magereza ili kubana matumizi ya serikali.
Masauni ameyasemahayo Leo katika ziara yake kutembelea Magereza ukonga ambapo amekagua Kiwanda cha Magereza cha kinachojishuhulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na nguo za askari Magereza.
Sanjari na hayo naibu waziri huyo ametoa wito kwa watanzania kwa kununuo bidhaa mbali mbali zinazo tengenezwa na magereza ilikuunga mkono kwa kazi nzuri wanazofanya.
Sanjari na hayo naibu waziri huyo ametoa wito kwa watanzania kwa kununuo bidhaa mbali mbali zinazo tengenezwa na magereza ilikuunga mkono kwa kazi nzuri wanazofanya.
Aidha amewapongeza askari wa jeshi la magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ilikumalizia maeneo machache yaliyo baki.
Naye kaimu Mkuu wa Magereza Kamishina msaidizi Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi kama machine za kushonea nguo, na mashineza za ufundiselemala , ukosefu wa mtaji wa kuendesha shughuli za kilimo hivyo amesema pindi serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine.
Post a Comment