Ads

TWAWEZA:IPATIKANAJI WA HUDUMA RASMI ZA KIFEDHA ZAONGEZEKA.


Mwambawahabari
Upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha nchini umeonekana kuongezeka kwa kiwango kikubwa hasa katika upatikanaji wa huduma za mikopo, bima na uwezo wa kutuma na kupokea pesa kwa urahisi na usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa makumbusho jijini dare s salaam mkurugenzi mtendaji wa Twaweza AIDAN  EYAKUZE amesema Utafiti huo umetolewa kupatikana sehemu salama ya kuhifadhia akiba kunasaidia kuwapunguzia watu ugumu wa maisha na kuwaongezera kipato chao.

Hata hivyo amesema huduma rasmi za kifedha zinashikiliwa na mitandao ya simu kwa asilimia kubwa ikiwa tafiti zinaonesha huduma hizo hutumika kwa kiasi kikubwa kwa utumaji na upokeaji wa fedha.


Amesema kuna ongezeko la asilimia 19 kutoka ilivyokuwa mwaka 2014  ambapo mwananchi mmoja kati ya watano yaani asilimia 22 ana akaunti yake mwenyewe benki au ya ushirika na mtu mwingine huku umiliki wa akaunti ukitofautiana kati ya tajiri  asilimia 56 na kaya masikini asilimia 6.

Aidha mkurugenzi huyo amebainisha kuwa wananchi wachache hutumia huduma za mitandao ya simu kuweka akiba ambao ni asilimia 22 au kulipia huduma mbalimbali ambao ni asilimia 11huku huduma za kibenki zikitumiwa zaidi na wananchi wa mjini amabao nisawa na asilimia 41 tofauti na asilimia 13 ya wananchi waishio vijijini

No comments