Ads

TIC KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI KWA NJIA ZA KISASA




Na John Luhende
mwambawahabari
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimeingia makubaliano na Oxford Business Group (OBG) ya Uingereza kwa ajili ya kufanya tafiti ya fursa zinazopatikana nchini ili kuandaa kitabu cha ripoti itakayotumika kutangaza fursa hizo dunia nzima.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika kituo cha uwekezaji jijini Dar es salaam,Waziri wa Viwanda,biashara na Uwekezaji Charlse Mwijage amesema kuwa Oxford Business Group ni manguli wa kufanya utafiti na biashara duniani hivyo watapita nchi nzima kuainisha fursa zilizopo na kuzitafutia uwekezaji.



Hata hivyo Waziri Mwijage amesema kuwa wawekezaji wengi kutoka Bara la Asia wanakuja Afrika kwa hiyo ni wakati mwafaka Tanzania iweke mazingira rafiki ili wawekezaji hao wapaone Tanzania kama sehemu iliyo salama kwa ajili ya kuwekeza.

Aidha amewataka watafiti hao kufanya utafiti ambao Tanzania isingeweza kufanya na utakapo kamilika wakazitangaze fursa sehemu nyingi duniani na kwa wafanya biashara wengi ambao Tanzania isingeweze kuwafikia.

Pamoja na hayo mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya uwekezaji Tanzania,Cliford Tandali amesema kuwa ubia walioingia na kampuni hiyo ni ubia wa manufaa na kampuni hiyo itakaa hapa nchini kwa miezi nane ikiwa itafanya kazi hiyo ya utafiti huku walengwa wakuu watakao hojiwa na viongozi mbalimbali wanao husika na sekta ya uwekezaji

No comments