TGNP YAFANYA MJADALA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA UKONGA
Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) leo hii umefanya mjadala wa kupinga ukatili katika kata za Kipunguni,Kivule na Mzinga ikiwa ni muendelezo wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika jimbo la Ukonga.
Aidha kaulimbiu ya kupinga ukatili huo ni“Funguka, Pinga Ukatili wa Kijinsia Elimu Salama kwa Wote.
Akizungumza katika mjadala huo uliofanyika kwenye kata ya Kipunguni B Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam Ofisa wa Program Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) Anna Sangaiamesema kuwa suala la Ukeketaji ni suala mtambuka
linalohitaji kupigiwa kelele kwa nguvu zote na watuwapatiwe elimu ili waelimike na waweze kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wasikiapo kuna vitendo vyaukatili wa kijinsia kama ukeketaji.
Pia wataweza kufahamu kuwa madhara ya ukeketaji ni makubwa na humpelekea msichana kuathirikakisaikolojia, pamoja na kupata maumivu makali,kuuguza kidonda, maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI, kutokwa damu kwa wingi, maradhi ya Fistula na huenda akafariki dunia.
Hata hivyo ofisa huyo amewataka polisi kutoa msaada pindi wanapoletewa taarifa za ukatili wa kijinsia kwani kumekuwepo na malalamiko kuwa wamekuwa wakipuuzia pindi wanapoletewa taariza hizo.
Huku Muwezeshaji Mshauri TGNP Agnes Lukanga ameeleza kuwa takribani wasichana 4000 kwa mwaka huu wamekeketwa hivyo ni vyema kila mmoja kujithamini ana nafasi gani katika kuleta mabadiliko kuhusu ukatili huo unaendele kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo Dodoma, Moshi, Arusha, na Tarime.
Kwa upande wake mwanaharakati Fatuma Abdulrahman ameeleza kuwa ni vyema wazee wa mila kwa makabila yanayofanya vitendo hivyo wapewe elimu ya kutosha kwani wananguvu ya ushawishi huku mwanaharakati mwingine Selemani Bishagazi akisisitiza elimu itolewe juu ya mila potofu na kasumba ya kusema usipo keketwa huolewi iondoke kwa makabila yanayofanya vitendo hivyo, huku wachangiaji wengine wakiwataka wazazi wa kiume na wakike washirikiane kwa pamoja katika mapambano ya ukatili wa kijinsia kwani bila wao hakuna mtoto atakaye keketwa au kufanyiwa ukatili wowote.
Click here to Reply or Forward
|
Post a Comment