Ads

SHUGHULI ZA CHAMACHA KUTETEA ABIRIA (CHAKUA) MIKOANI ZASITISHWA

Image result for picha za kamanda mpinga

Na Maria Kaira
mwambawahabari
Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Mohammed Mpinga amesitisha leo hii utendaji wa chama cha kutetea abiria(CHAKUA)kutojihusisha na usimamizi wa sheria ambazo zinahusiana na jeshi la polisi katika vituo vikuu vya mabasi vya mikoani na badala yake watabaki katika kituo kikuu cha mabasi ubungo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda Mpinga amesema chama hicho kitaweza kuruhusiwa kutoa elimu katika vituo vya mabasi  vya mikoani hadi watakapopata idhini kutoka kwa makamanda wa polisi wa mikoani.


"Kutokana na utendaji wao umekuwa mbaya kiasi kwamba wanakiuka maadili na kujikita katika usimamizi wa sheria badala ya kutoa elimu kuanzia sasa nasitisha utendaji wa CHAKUA mikoani,pia wajihusishe na utoaji elimu tu wasijihusishe na usimamizi wa sheria ambalo ni jukumu la jeshi la polisi" amesema

Pia ametoa wito kwa madereva wote nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima ambapo amewataka abiria kupaza sauti pindi wanapoona dereva anaendesha mwendo kasi.

Aidha Kamanda Mpinga amesema madereva wote watakao kiuka sheria za usalama za barabarani watachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwa pamoja na kuwapeleka mahakamani, ambapo wataendelea na operesheni ya ukaguzi wakushitukiza kwa kuwapima madereva ulevi na kuwakamata.

"Natoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajari,nawaomba wazazi na wananchi kwa ujumla kuangalia usalama wa watoto wao wanapovuka barabara,pia katika kumbi za Disko na fukwe za bahari jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani tutaongeza nguvu za kutosha katika kipindi hiki" amesema

Hata hivyo ameongeza kuwa vyombo vyote vya moto vilivyokuwa na taa za mwanga mkali vinatakiwa kuondoa taa hizo Mara moja ikiwa watakiuka agizo hilo hatua Kali zitachukuliwa juu yao.

No comments