JESHILA POLISI LAWAONYAWAMILIKI WAKUMBI ZA STAREHE KUTOJAZA WATU SIKU YA SIKUKUU ZACHRISTMAS
Na Maria Kaira
mwambawahabari
Jeshi la Polisi Tanzania limewataka wamiliki wa nyumba za starehe hapa nchini kuacha kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu hadi kupita kiasi katika kumbi hizo na badala yake kuwataka wazingatie uhalali wa matumizi ya kumbi zao katika kipindi cha sikukuu.
Akizungumza na waandishi wa habari kamishina msaidizi wa polisi( ACP) Advera Bulimba amesema katika kuelekea kwenye kipindi hiki cha sikuu za Krismas na Mwaka Mpya, jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha kwamba wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bila ya kuwepo kwa vitendo vyovyote vya uhalifu.
"ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya ya watu hivyo wananchi wasiwe na shaka kwa hilo usalama umekamilika pia wananchi tushirikiane kutoa taarifa pindi waonapo vitendo vya uharifu" amesema
Pia amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao ili kuepuka upotevu wa watoto, ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara katika siku za sikukuu.
Aidha amewashauri wamiliki wa maduka makubwa kufunga kamera za CCTV ili kuweza kurekodi mienendo ya watu wanaingia na kutoka kwenye maduka yao ili kuweza kubaini uhalifu unaojitokeza kwa haraka katika maduka hayo.
"Tunawahakikishia wananchi kwamba jeshi la polisi linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi na hivyo halitawajibika kumwonea huruma au kumpendelea mtu yeyote atakaye enda kinyume na sheria" amesema
Post a Comment