Ads

Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) laipongeza TGDC


Displaying IMG_2232.jpg

Na. Johary Kachwamba - TGDC
Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) laipongeza Taasisi ya nishati ya joto ardhi nchini (TGDC) kwa jitihada walizofikia na kuahidi kuendeleza ushirikiano nao.

Pongezi hizo zimetolewa na Mtaalamu wa Nishati kutoka Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia Dkt. Thrainn Fridrikson wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati ya joto ardhi nchini iliyoendeshwa na wataalamu kutoka Chama cha Kimataifa cha Joto ardhi (International Geothermal Association – IGA) mapema wiki hii.


‘Nina imani kubwa na uelewa mlionyesha katika semina hii kuwa mtakuwa mmepata elimu yakutosha itakayowasaidia katika uvumbuzi wa nishati hii ya joto ardhi lakini pia mafunzo haya yatasaidia kurahisisha shughuli zenu na kupelekea uzalishaji wa nishati hii kuanza mapema hapanchini, alisema Dkt. Fridrikson.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Meneja Mkuu (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka alitoa shukrani kwa ESMAP na kusema ni fursa muhimu kwa TGDC kama kampuni katika maandalizi ya kuendeleza nishati ya jotoardhi inayolenga kusaidia taifa kufikia malengo yaliyo katika dira ya 2025.

Kwa upande wake Mhandisi Uchorongaji, Amani Christopher kutoka (TGDC) alisema kuwa mafunzo yamewaongezea utaalamu katika utekelezaji wa kazi zao za kitafiti na wanatarajia kufanya kazi kwa wepesi zaidi tofauti na awali kwani mafanzo hayo yamewaongezea uelewa katika sekta hiyo.

Mafuzo hayo ya siku nne yalijikita katika kuwajengea uwezo wahandisi wa uchorongaji, pamoja na sekta nyingine kama usimamizi manunuzi, taratibu za kisheria, na Usimamizi wa fedha za kugharamia miradi.




No comments