JAFO ;WATUMISHI FANYENI KAZI ACHENI KUWAZA KUTUMBULIWA
Na.John Luhende
mwambawahabari
Naibuwaziri
wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh Suleiman Jafo amewataka watumishi
wa waumma kufanya kazi kwa kujiamini
katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta mabadiliko ya
kimaendeleo katika Taifa.
Mh Jafo
ameyasema hayo leo wakati akizungumza na
watumishi wa umma wa manspaa ya Ilala na
jiji la Dar es slaam watendaji ,wabunge
pamoja na madiwani na kuwa elekeza wakuu
wa idara kufanya kazi na kuwapa ushirikiano watumishi wangazi za chini
katika idara zao na kuacha kuwanyanyasa .
‘’Nawaagiza
wakuu wa idara muache kuwa nyanyasa
watumishi walio chini yenu kwakuwa wengi wanafanya kazi kwa hofu ya kuogopa
kutumbuliwa nakupelekea kutokuwa na
amani katika maeneo yao ya kazi.’’ Alisema Jafo
Aidha
amesema wizara yake itatoa ushirikiano kwa
watumishi wote wanaotekeleza majukumu yao
kwa moyo na bidii na amewaagiza wakuu wa idara kuwa na utaratibu wa kutambua
kazi za watumishi wanao jituma na kuvuka malengo ya kazi walio wekewa hatakama hakuna pesa za kuwapa angalau waandikiwe barua ama kupewa vyeti vya
kutambua michango yao mahala pa kazi
Hata hivyo
ame mpongeza mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam , mkurugenzi wa jiji pamoja na madiwani
kwa kusimamia suala la usafi wa jiji kwakuwa kusimamia usasafi japo
kuna baadhi ya maeneo machache ambayo
bado ya naonekana kulalamikiwa na
wananchi
‘’Zamani
jiji la Dar es salaam lilikuwa
chafu lakinikwa sasa hali imekuwa nzuri ukilinganisha na kabla ya
kampeni ya usaf iliyo anzishwa na Rais
tarehe 9 Disemba mwaka jana’’ alisema Jafo
Pamoja na hayo
mh Jafo ameuagiza uongozi wa manispaa ya
ilala kwa kushirikiana na katbu tawala mkoa
wa Dar es salaam kupitia upya mkataba alio pewa mpangaji katika
eneo lilo tolewa na Dawasco kwa ajili ya kujenga shule ya kata ya secondary Buguruni
kutembelea eneo hilo na kisha
kufanya maamuzi ili eneo hilo liweze kujengwa shule.

Post a Comment