MWENYEKITI MPYA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI SEMISTOCLES KAIJAGE AANZA KAZI RASMI.
Mkurugenzi wa Uchaguzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto) akimkaribisha
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa,
Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi za Tume zilizoko Posta
jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini
Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5.
Watumishi wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara
baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar
es salaam.
Mwenyekiti mpya wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji
Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada
ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo
kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mwenyekiti mpya wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji
Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ofisini kwake.
Mwenyekiti mpya wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji
Semistocles Kaijage akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya Habari kuhusu majina 11 yaliyoteuliwa kugombea Ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani Zanzibar
na majina 72 ya wagombea Udiwani kwenye
Kata 20 za Tanzania Bara. Picha/Aron Msigwa -NEC
Post a Comment