Ads

MSHINDI WA SHINDANO LA USHAIRI LA MEYA WA JIJI LA DSM APATIKANA . SOMAHAPO UMFAHAMU.



Na Maria Kaira
mwambawahabari
Hatimaye Dotto Rangi Moto ameibuka kuwa  mshindi wa kwanza katika tunzo ya pili ya ushairi ya mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam, huku akiibuka kidedea na utunzi wake wa shairi lijulikanalo mwanangu rudi nyumbani lililoweza kumpatia ushindi.

Shindano hilo lilikuwa la aina yake, lililofanyika leo katika viwanja vya karimjee jijini hapa ambapo jumla ya washiriki 40 waliweza kushiriki kwenye tuzo hizo na hayimaye kuibuka kumi bora na kubaki tatu bora na kuweza kujinyakulia zawadi zao.




Aidha mshindi wa pili katika tuzo hizo ni  pamoja na  Omary Bakari aliyetunga shairi lenye kichwa cha KICHAPWI,wimbi kuu na kufatiwa na Nasoro Mohamed aliyeshika nafasi ya tatu.

Hata hivyo katika mashindano hayo mshindi wa kwanza amekabidhiwa kiasi cha fedha taslimu sh. Laki Tano, mshindi wa pili amekabidhiwa sh.tatu na mshindi wa tatu amekabidhiwa sh. laki mbili.

Sanjari na hayo zawadi hizo  zimekwenda sambamba na washindi wa nafasi ya nne hadi 10 ambapo kila mmoja amepatiwa  zawadi ya shilingi 100, 000 taslimu ikiwa kama motisha ili waweze kufanya vizuri katika shindano lijalo.



Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa shindano hilo, Chata Michael amesema washiriki wote walioshiriki katika kinyang'anyiro hicho ni washindi, wasikate tamaa pia lengo lao la kuanzisha shindano hilo litakuwa endelevu na kuwataka watanzania kushiriki kwa wingi pindi watakapo tangaza tena.


Hata hivyo mmoja wa washiriki aliyeweza kuingia kumi bora sikudhani jalala amewasihi wenzake kutokata tamaa na matokeo waliyopata na kuwataka wajipange umpya katika shindano lingine litakalo la msimu wa tatu.

No comments