MEYA WAJIJI LA DSM AWATAKA WATANZANIA KUPENDA KUTUMIA LUGHA FASAHA YA KISWAHILI.
Na Maria Kaira
mwambawahabari
Watanzania wameshauriwa kupenda na kutumia lugha fasaha ya kiswahili kama nyenzo tosha ya kuhakikisha lugha hiyo inakuwa na kuimarika hapa nchini, pamoja na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo hii Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema watanzania wengi wamekuwa wakidharau lugha ya kiswahili na badala yake kupenda lugha za kigeni na kuachana na lugha yao kwa kujihisi kuonekana washamba kwa kutokujua lugha za kigeni.
"Sisi wenyewe tumeamua kuwa watumwa katika nchi yetu, nakuanza kutumia lugha za kigeni na kusahau lugha yetu,mtu akiona anaongea kiswahili anajiona mshamba, tunaona nchi za wenzetu wanathamini sana vyakao na sisi tujitahidi kuipenda lugha yetu" amesema.
Aidha Mwita ameshauri lugha hiyo iweze kutumika ipasavyo kwa wazawa wenyewe nasio kuwaachia mataifa mengine kuitumia, Pia amesema watao uamuzi watoe uamuzi ili lugha hiyo ya kiswahili iweze kutumika kama lugha ya kufundishia kuanzia kidato cha kwanza hadi Chuo kikuu.
"Tuna kila sababu ya kuhakikisha lugha ya kiswahili inaendelea kuenziwa hapa nchini kama lugha yetu ya taifa pamoja na kuiendeleza ili iweze kutuletea maendeleo, kiswahili ni mtumwa wa moyo kimebeba kila kitu" amesema
Hata hivyo jaji wa shindano la tunzo ya mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam ambaye alikuwa waziri wa zamani katika wizara ya habari utamaduni na michezo Mohammed Seif Hatibu amewasihi watanzania kupenda na kuchangamkia kiswahili na kuachana na lugha za kigeni na kusahau vya kwao.
"Lazima watanzania tufike mwisho kupenda vya wenzetu,Tuige mfano kwa rais wa awamu ya tano anavyothamini lugha ya kiswahili, nawapa hongera viongozi wote wanaotumia lugha ya kiswahili pia watanzania tumeunganishwa na kiswahili lazima tukipende na kukitumia" amesema
Post a Comment