MAKONDA KUGHARAMIA MATIBABU YA MTOTO ALIYE TELEKEZWA,A AHIDI KUTOA MILIONI MOJA KILA MWEZI.
Na MariaKaira
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kutoa msaada wa sh. Milioni 1 kila mwezi kwa mtoto Alex Komba mwenye matatizo ya uvimbe kichwani hadi atakapo fanikiwa kupatiwa matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kutoa msaada wa sh. Milioni 1 kila mwezi kwa mtoto Alex Komba mwenye matatizo ya uvimbe kichwani hadi atakapo fanikiwa kupatiwa matibabu.
Alex ambaye analelewa na baba yake mzazi Andrew Komba, alikimbiwa na mama yake mzazi mwaka mmoja uliopita baada ya kupatwa na ugonjwa huo, alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kufanyiwa matibabu lakini ilishindikana kutokana na mzazi wake kukosa fedha na kusababisha mzazi huyo kubisha hodi kwa Makonda kwa ajili ya kumuomba msaada
Wakati akimkabidhi, fedha taslimu 200,000 baba mzazi wa mtoto huyo, Makonda amesema ahadi hiyo anaanza kuitekeleza kuanzia mwezi huu.
" Jumatatu ijayo njoo ofisini kwangu uanze kuchukua fedha niliyokuahidi," alisema Makonda.
Komba alimshukuru Makonda kwa msaada huo na kuwataka wazazi na walezi wenye watoto wenye matatizo kutowaficha.
"Nilimpeleka mtoto wangu Muhimbili wakaniambia ana tatizo la uvimbe kichwani ingawa hakuzaliwa na ugonjwa huo. Mama yake mzazi alimkimbia, kwa sasa namlea mwenyewe Kutokana na hali ngumu kiuchumi wakati mwingine naenda nae kibaruani sababu hawezi kufanya chochote na ni mdogo," amesema na kuongoza.
"Mungu aendelee kumtunza katika mambo yake, na pia nawashauri wazazi au walezi wenye watoto ambao wana matatizo kama haya kutoficha watoto zao nyumbani bali wawatoe ili wapatiwe msaada."
Post a Comment