VITUO 20 VYA POLISI KUJENGWA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Maria Kaira
Mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza kuanza mchakato wa ujenzi wa vituo 20 vya polisi vitakavyogharimu jumla ya sh. Bilioni 10 ili kupunguza Changamoto kwa wananchi.
Hatua hiyo imetokana na Mkuu huyo kupokea malalamiko na changamoto mbalimbali kuhusu hali ya huduma za kipolisi katika mkoa wa Dar es salaam,ikiwa ni pamoja na mazingira mabovu na yasiyoridhisha ya vituo vya polisi na wanachi kutopatiwa huduma kwa saa 24 kutokana na vituo hivyo kufugwa wakati wa usiku.
Kwa taarifa iliyotolewa na Mkuu huyo amesema kila kituo kimoja kitatumia sh. Milioni 500 pesa ambazo anampango wa kufanya mazungumzo maalumu na wadau wa maendeleo wa mkoa wake ili kuweza kufanikisha ujenzi huo.
Makonda amesema kila wilaya itaweza kujenga vituo vinne vya polisi na kila kituo kitakuwa na ofisi ya kisasa pamoja na vyumba vitatu vya maabusu kwa wanawake na wanaume, pia Kila kituo kimoja kitatumiwa na askari wasiopungua 100.
" Nazitaka kamati za ulinzi na usalama za wilaya zote wa mkoa wa Dar es salaam kupeleka mchanganuo wa maeneo ambayo vituo hivyo vitajengwa ili kuwarahisishia wananchi kupata hiduma za ulinzi na utulivu katika mkoa wa Dar es salaam" amesema
Pia ametoa onyo kuzuka kwa tabia mbaya kwa baadhi ya viongozi na wananchi kutaka kupata faida kwa kuchapisha fomu na kupitisha kwa wananchi kwa madai ya kuchangisha mchango huo.
" Fomu hizo ni batili na watu hao ni waongo wakipatikana wanafanys hivyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yao kwa kuwa hawajatumwa na mtu yoyote"amesema
Post a Comment