Shindano la ushairi la Meya wa jiji kuanza Desemba 10
mwambawahabari
Na Christina Mwagala,
Dar es Salaam
MASHINDANO ya pili ya
tuzo ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita la uandishi wa
ushairi linatarajiwa kuanza Desemba 10 hadi 13 mwaka huu katika viwanja vya
Karimjee.
Mratibu wa mashindani
hayo Chatta Michael amesema kwamba lengo la mashindano hayo ni kutoa fursa kwa
washiriki wa Kiswahili kushiriki katika kutafakari hali na maendeleo ya jiji
kwa kutumia sanaa yao.
Amesema kwamba mbali
na hilo, pia ni kuienzi historia ya jiji sambamba na kutambua mchango wa meya
wa kwanza Mwafrika hayati Sheikh Kaluta Amri Abeid ambaye enzi zauhai wake
alikuwa mshairi.
“ Mashindano haya
tunawapa fursa pia ,kuijadili Dar es Salaam hali na mstakabali wa jiji lao na
hivyo kuchangia katika kuhamasisha maendeleo ya jiji hili,na lugha ya
kiswahili.
“ Kufufua sanaa ndani
ya jiji, ili litumike kwa burudani ,elimu na maendeleo ya wakazi wote wa hapa,
kuendeleza vipaji vya washairi wakongwe sambamba na kuibua vipaji vya washairi
vijana ambao watakuwa ni wapya” amesema Chatta.
Aidha amefafanua
kwamba mashindano hayo yataanza Desemba 19 hadi 20 mwaka huu ambapo washindi
wata tangazwa na hivyo mshindi wa kwanza atapatiwa shilingi 500,000, wapili
shilingi 300,000, huku washindi nane wakipatiwa zawadi ya shilingi 100,000 kila
mmoja.
Alisema mada kuu
katika ushairi huo ni “Jiji la Dar es Salaam” ambapo mshairi atatakiwa kujadili
mada ndogo inayohusiana na mada kuu, ikiwemo historia ya jiji, jiografia,
utamaduni ,uchumi, mazingira ,sanaa na lugha .
Mbali na hivyo, lakini
pia kueleza changamoto zilizopo katika jiji ,raha na karaha ,maendeleo wananchi
wanaoishi katika jiji hili ambapo kila shairi litatakiwa kuzungumzia mada ndogo
tofauti.
Hata hivyo mashindano
hayo hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu yalifanyika Julai na kushirikisha
washiriki 20 ambao washindi wa kwanza walipatiwa zawadi ya shilingi 500,000.
Post a Comment