NAPE :SERIKALI INADHAMIRA YA DHATI KUIMARISHA MICHEZO NCHINI
Na Maria Kaira
Mwambawahabari
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imesema imedhamiria kuimarisha michezo hapa nchini ikiwa na lengo la kuboresha uchumi, afya na Maisha ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Pia itaendelea kuhakikisha sekta hiyo ya michezo inaendea na kukua katika maeneo yote bila kujali jiographia ya eneo husika kwa kuwa Tanzania ni moja.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo hii Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa kupokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Star times
Tanzania amesema anatoa wito kwa wadau na wapenda michezo kuendelea kusaidia kwenye tasinia ya michezo kwa kuchangia vifaa ili taifa liweze kuwa na uhakika wa kuwa na timu imara.
Tanzania amesema anatoa wito kwa wadau na wapenda michezo kuendelea kusaidia kwenye tasinia ya michezo kwa kuchangia vifaa ili taifa liweze kuwa na uhakika wa kuwa na timu imara.
" Serikali ni wajibu wetu kuhakikisha vifaa vilivyotolewa vinawafikia wananchi ili waweze kuvitumia hatimaye kukuza tasnia ya michezo nchini ambayo sasa imekuwa mchango mkubwa katika soko la ajira kwa vijana nchini" amesema
Pia Waziri Nape amesema baada ya kumaliza kuteng'eneza mswada wa Habari anatarajia kuteng'eneza Mswada mwingine wa Michezo ilikuweza kuondokana na tatizo la vilabu vya michezo kupeleka migogoro yao mahakamani.
Waziri Nape amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya vilabu vya michezo hapa nchini kutafuta suluhisho mahakamani pindi vinapopata migogoro kwenye vilabu vyao ambapo nikitu kisichopendeza.
''Tunataka tudhibiti watu kwenda mahakamani hasa vilabu vya mpira kwani mahakama sio mahala pazuri suala la taasisi yoyote ya kimichezo mahakamani kunaondoa sura ya Michezo ''Alisema Nape .
Kwaupande wa mkurugenzi kutoka Star Times Tanzania Juma Sharobaro amesema wametoa mipira 100 na T-shirt 100 kwa lengo la kukuza na kuendeleza vibaji vya wachezaji kuanzia ngazi za chini hasa maeneo ya pembezoni mwa nchi.
Post a Comment