17 WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUPIGA TRAIN MAWE ,NA KUHUJUMU RELI NA KUJERUHI MFANYAKAZI WA TRL.
Na Maria Kaira
Mwambawahabari
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma na ghasia katika miundombinu ya reli na treni vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imetoa onyo kwa wananchi kuachana na vitendo hivyo Mara moja.
Na badala yake kufuata sheria na taratibu za kutumia huduma hizo za treni na kuacha kujihusisha na vitendo vya uharibifu wa treni .
Akizungumza na waandishi wa habari jiji hapa Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Masanja Kadogosa amesema mnamo Novemba 7, 2016 treni ya mizigo ya Pugu kupata ajali, baadhi ya watu walifanya fujo kwa kurusha mawe na kubaribu mabehewa saba pamoja na kujeruhi wafanyakazi wake.
Pia Kadogosa amesema anatoa tahadhari kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara pembezoni mwa reli hizo kutoa taarifa za uhalifu zinazojitokeza,pia amesema kuwa wasipotoa taarifa za watu wanaofanya uharibifu wa miundombinu hiyo wataondolewa katika maeneo hayo.
Aidha hatua hiyo imefikiwa baada ya kutokea zaidi ya matukio matatu ya uharibifu wa miundombinu ya treni za TRL ikiwa tukio la mara ya kwanza lilijitokeza tarehe 24, 26 na 28 mwezi wa October na Novemba 7 Katika matukio hayo kulitokea uharibifu wa miundombonu na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi wa TRL.
" Pia kutokana na uharibifu huo uliojitokeza watuhumiwa 17 wanashikiliwa na jeshi la polisi pindi upepelezi utakapo kamilika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao wanaohusika na fujo na uharibifu huo ni makondakta wa dalala kwa lengo la kutisha wananchi kutoutumia usafiri wa treni" amesema
Hata hivyo Kadogosa ameongeza kuwa hawataweza kusitisha huduma hiyo kutokana na wananchi wengi wananufaika na huduma hiyo.
Kwa upande wa Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Reli, Simon Chillery amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wengine waliohusika na kitendo hicho na kuwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
" Huduma hii ilianzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi ili kuondokana na foleni za hapa na pale tunasikitishwa na hivi vitendo vinavyojitokeza kwa hivi sasa" amesema
Naibu Kamishna chillery ametoa wito kwa wanachi kuheshimu mali za umma na kuwa na moyo wa kizalendo wa kulinda rasilimali za serikali.
Post a Comment