WAZAZI WAPENI WATOTO HAKI YA KUPATA ELIMU
Na Maria Kaira
Mwambawahabari
IKIWA tatizo la ndoa za utotoni linazidi kukithili nchini, wazazi,walezi na jamii wametakiwa kuhakikisha wanawapatia watoto wao haki ya kusoma, kuishi na kuwalinda dhidi ya ndoa za utotoni.
Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Magreth Mussai amesema kila mtu awajibike kuhakikisha mtoto wa kike haolewi katika umri mdogo.
Magreth amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika Octoba 11 mkoani Shinyanga huku yakiwa na lengo la kuelimisha na kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutetea haki za watoto Wa kike.
Pia maadhimisho hayo yataenda sambamba na kaulimbiu isemayo "mimba na ndoa za utotoni zinaepukika chukua hatua kumlinda mtoto wa like"
"Tumeamua kuanzia mkoani shinyanga kwasababu ndio mkoa unaongoka kwa asilimia 59 , tatizo hili linatokana na baadhi ya familia kuwa na umasikini uliokithiri"amesema
Aidha serikali kupitia maadhimisho hayo wwtatumia kuelimisha jamii kutambua kwamba kumuozesha mtoto wa kike nchini ya umri wa miaka 18 unakuwa unamuathiri kisaikolojia.
Mhadhiri kutoka Agaknan University Veronica Sarungi amesema mtoto chini ya miaka 18 anakuwa bado hajamudu majukumu ya kifamilia na uzazi, anatakiwa kupatiwa elimu na stadi za Maisha.iz
Post a Comment