Ads

WATAKIWA KUTUMIA UTAFITI WA URAGHABISHI ILI KUKUZA UCHUMI,NA KULETA MAENDELEO





Na Maria Kaira
Mwambawahabari
JAMII imetakiwa kutumia dhana ya  utafiti wa uragabishi ili kuweza kuistua jamii kujitambua na kukua kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi,kimaendeleo na kijamii.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mtandao wa Tgnp,Lilian Liundi wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na Mtandao huo kufanya utafiti  wa Uraghabishi kuwa umesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mwamko katika wilaya Saba ambazo wamezifanyia utafiti huo.

Pia Liundi amesema utafiti  wa uragabishi umechangia kuleta mabadiliko makubwa ya Kimaendeleo katika jamii inayowazunguka tofauti na mwanzoni.

"mfumo  huu mpya tunaotumia kutoa elimu kwa wananchi  ni jinsi gani wataweza kushirikiana na viongozi wao katika harakati za kujipatia maendeleo  mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kuhoji maswala mbalimbali kwa viongozi wao nakujua ambavyo walikuwa hawavijui (Uraghibishi), umeweza kuleta maendeleo makubwa katika jamii kuzitambua nafasi zao" amesema

Liundi amesema mfumo huo mpya wa uraghbishi ulianza tangu mwaka 2012  na waliweza kuzifikia wilaya saba ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Kisarawe, Mororgoro vijijini,Mbeya vijijini na Kishapu huku  pia wakiweza kuvifikia vikundi zaidi ya 222,wakiwemo wanaume zaidi ya 1000 na wanawake zaidi ya 3000 huku akisema kuwa zoezi hilo linaendelea ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.

Pia ameeleza kuwa njia hiyo imefanikiwa  kwa kiwango kikubwa kuleta maendeleo kwa  wananchi wengi ambao hawakujua nini wanatakiwa kufanya endapo serikali itakwama katika kuwaletea maendeleo.
Mmoja wa wananchi Asha Rajabu anatoa wito kwa shirika hilo na mashirika mengine kuendelea kuelimisha jamii kuhusiana na mfumo huo mpya ili jamii iweze kutambua haki zao na kuacha dhana ya kuwaogapa viongozi wanaowaongeza.

No comments