SMBA CHAWENE ANG,AKA WALIOVAMIA MAENEO YA TAASISI ZA UMMA, A AGIZA WAONDOLEWE

Na Maria Kaira Dar
mwabawahabari
Kutokana na kukithiri kwa uvamizi wa maeneo ya taasisi za kiserikali yakiwemo ya shule za msingi na sekondari, vituo vya kutolea huduma za afya, hospitali na masoko unaofanywa na baadhi ya watu kwa kujenga nyumba za makazi na vyumba vya biashara.
Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, leo ametoa agizo kwa Maafisa Ardhi na Wakurugenzi walio chini ya mamlaka ya TAMISEMI kupima mipaka halisi ya maeneo ya taasisi hizo pamoja na kuwaondoa watakao bainika kuyavamia maeneo hayo.
Simbachawene ametoa muda wa miezi mitatu kwa maafisa ardhi hao,ili waweze kukamilisha zoezi hilo la upimaji, pia ametoa maagizo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia zoezi hilo ili likamilike kwa wakati.
Pia lipo tatizo kubwa la uvamizi wa maeneo ya kutolea huduma za kiserikali ambapo watu wanafanya ujenzi wa nyumba na vyumba vya biasara kwa ajili ya kujipatia kipato. Ziko shule ambazo maeneo yake yanakaribia kupotea, bahati mbaya hayo maeneo wataalamu wa ardhi wana mamlaka nayo wenyewe na hawayafanyii upimaji.
Aidha, amepiga marufuku ujenzi wa vyumba vya biashara katika shule, masoko na hospitali za serikali kwa vigezo kuwa ni vyanzo vya mapato kwa kuwa vinaathiri muingiliano wa kiutendaji na utoaji huduma wa taasisi hizo.
"Ujenzi wowote uliopo na unaotarajia kufanywa uthitishwe kuanzia sasa," amesema.
Simbachawene ametoa agizo kwa walioingilia katika mipaka ya maeneo ya taasisi za serikali, waondoke wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
"Wananchi waliovamia maeneo ya taasisi hizo waondoke wenyewe vinginevyo hatua za kuwaondoa kwa nguvu zitatumika.Mfano soko la Tandale karibu linapotea kutokana na kuvamiwa na watu, natoa wito kwa jamii iliyozunguka maeneo hayo kutoa taarifa kwa mamlaka za serikali za mitaa wanapobaini kuna uvamizi wa maeneo unatendeka," amesema.
Post a Comment