Ads

MWAKYEMBE AMTAKA DPP KUWAKOMALIA WALIO UWA WATAFIT


Displaying 1.jpg
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Harrison Mwakyembe akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mauaji ya wataalamu wa utafiti yaliyotokea hivi karibuni mjini Dodoma, kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Bw. Amon Mpanju. (Picha na Benjamin Sawe)

Na Maria Kaira Dar  
mwambawahabari
Wizara ya  Katiba na Sheria imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)  kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kujihusisha kikamilifu na upelelezi wa kesi ya mauaji ya wataalamu wawili wa utafiti wa udongo na dereva mmoja, yaliyotokea hivi karibuni katika kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma.


Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema wizara yake itahakikisha kuwa wote waliohusika kufanya tukio hilo la mauaji wanafikishwa mahakamani.

Pia amesema Jamhuri itahakikisha inadai adhabu kali kwa kila mtuhumiwa ili kutoa fundisho kwa wananchi wote kwamba tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kigezo cha hasira kali hakifai.

"Wizara itachukua kila hatua ili kuweza kukomesha kabisa wimbi hilo la  wananchi kujichukulia sheria mkononi ,  kwa waliohusika kushawishi, kuhamasisha, au kuchochea ,kupanga, kushambulia kwa mapanga na kushiriki kuchoma moto katika tukio hilo wanafikishwa mahakamani kuvuna walichopanda," amesema.


Dk. Mwakyembe amesema wizara inashtushwa na ongezeko la matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa visingizio mbalimbali.

"Wengi wanafanya matukio hayo kwa visingizio mbalimbali kama kukasirishwa na baadhi ya matukio wanayoyaona mabaya, kuhisi kuonewa, kuchoshwa na michakato halali ya kisheria ya upelelezi, uendeshaji kesi na utoaji hukumu," amesema.

Hata hivyo amevitaka vyombo vya habari kuisaidia serikali katika kampeni ya kutokomeza vitendo vya wanachi kujichukulia sheria mkononi.

No comments