Ads

BANK YA TWIGA YAFILISIKA ,BOT YACHUKUA USIMIMIZI .

Mwambawahabari
Displaying 1..JPG
  1. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndullu (kulia) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuivunja Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti ya Uongozi wa Benki ya Twiga Bancorp kuanzia leo Ijumaa tarehe 28 Oktoba, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa usimamizi wa mabenki, Kennedy Nyoni.
Displaying 2..JPG

  1. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndullu (kulia) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuivunja Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti ya Uongozi wa Benki ya Twiga Bancorp kuanzia leo Ijumaa tarehe 28 Oktoba, 2016. Kulia ni Kaimu Katibu wa Benki Kuu, Mustafa Ismail.

Displaying 3..JPG
  1. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndullu (katikati) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuivunja Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti ya Uongozi wa Benki ya Twiga Bancorp kuanzia leo Ijumaa tarehe 28 Oktoba, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa usimamizi wa mabenki, Kennedy Nyoni na kulia ni Kaimu Katibu wa Benki Kuu, Mustafa Ismail.



Displaying 4..JPG

  1. Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wa Gavana ya Benki ya Tanzania, Prof. Benno Ndullu kuhusu uamuzi wa  Serikali kuivunja Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti ya Uongozi wa Benki ya Twiga Bancorp kuanzia leo Ijumaa tarehe 28 Oktoba, 2016.

(PICHA NA MAELEZO)

Na Beatrice Lyimo

SERIKALI kupitia Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeamua kuchukua usimamizi wa benki ya Twiga baada ya kubaini benki hiyo kuwa na upungufu wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa Benki ya kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndullu alisema kuwa upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake. 

Akifafanua zaidi Prof. Ndullu alisema uamuzi huo umetokana na mamlaka ya Benki kuu ya Tanzania iliyopewa chini ya kifungu cha Sheria namba 56(1) (g) (i)na 56(2) (a)-(d) cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

“Uamuzi huu umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki ya Twiga ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake hivyo kutoa huduma kwa benki ya twiga kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake, alifafanua,” Prof Ndullu.

Kutokana na uamuzi huo, Prof Ndullu alisema BOT imeamua kuisimamisha Bodi ya wakurugenzi na Menejhimenti ya benki hiyo na kuteua Meneja Msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughiuli za benki kwa kipindi ambacho kitakuwa chini ya usimamizi wa Benki kuu.

“Benki kuu ya Tanzania haina nia ya kukaa na kuendesha benki hiyo kwa muda mrefu, nia ni kuweza kupata suluhu ya kupata wawekezaji wengine watakaoendesha shughuli hizo” alisema

Prof Ndullu alisema katika kipindi kinachokadiriwa kufika wiki moja kuanzia leo Octoba, 18 mwaka huu shughuli za utoaji wa huduma za kibenki za benki ya Twiga zitasimama ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga taratibu za uendeshaji huo.

Aliongeza kuwa pamoja na mabadiliko hayo,  BOT inawahakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilifu katika sekta ya fedha.

No comments